Kama una mwanamke wako, ni mke wako, mpenzi au mchumba wako na unampenda, muonyeshe kuwa unampenda, si uanaume kumtukana, si uanaume kutokujibu meseji zake, si uanaume kumpiga, si uanaume kumdhalilisha mbele za watu. Mwanamke anaweza kuvumilia ujinga wako wote lakini kumbuka kuwa siku akichoka hutamuona, hata manyoya ili kujua aliliwa wapi hutayaona, narudia kama unampenda na unamfanyia vituko kwakua unadhani kuwa ni uanaume basi si unaume ni ushamba.
Kama unafanya hivyo vituko hakikisha kuwa humtaki kweli na si unatingisha kiberiti, nikuambie tu kuwa siku akipata fala mwingine ambaye atamsifia, ambaye atajibu meseji zake, ambaye atamuuliza kaamkaje, ambaye hatamtukana na kumfanyia hayo unayomfanyia nakuambia kua hutamuona, hatajali tena na najua unajiambia wanawake wapo wengi naweza kumpata yoyote lakini nikuambie kitu kuachwa kunauma, tena kama ulikua ujajishaua kuwa haendi popote unaona kachukuliwa na mshikaji ambaye ulikua unamchukulia poa?
Kachukuliwa na ananawiri kiasi kwamba hata kukukumbuka hakukumbuki inauma sana na najua utajikaza kiume lakini maumivu yake ni kama kaondoka na nguvu zako za kiume, kwamaana ulikua unampenda ila ulikua unajifanya tu kidume kuigaiga ya watu, ulikua unajifanya kana kwamba hujali kwakua unahdani haendi popote, ndugu yangu ataenda na akiondoka utajikuta unahangaika kubadilisha wanawake kama nguo, unajikuta unahangaika kufanya kila kitu ili kurudisha mambo kama zamani lakini hayatarudi hivyo kama unampenda muonyeshe kabla lijamaa tu huko mtaani halijaanza kumuonyesha!
Like
Share
Like
Share
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/kama-una-mwanamke-wako-ni-mke-wako.html
No comments:
Post a Comment