Monday, March 30, 2020

Unaweza kuwa Unaumia sana muda huu. Lakini itafika siku ambapo hutajali tena.


.
Itafika siku moja utapitisha siku nzima bila ya kumpigia simu au ku-mtext na kujiona uko sawa kabisa.
.
Itafika siku utasikia yupo na mtu mwingine na wala hutahisi kuumia au kukasirika.
.
Itafika siku moja, utaziona picha zake na wala hutajihisi jambo lolote. Unaweza kutana nae ukaongea nae na zile hisia za kuumiza juu yake hutazihisi tena.
.
Najua, unaweza usiamini ninachokiongea kutokana na tabia ya moyo ya kung'ang'ania, lakini, fahamu kwamba, muda nao huponya. Haiwezi kuwa hivi sasa, ila siku itafika tu.
.
Na siku hiyo itakapofika, utajishangaa kwanini ulikuwa ukilia? Kisha, utaona uamuzi wa kumuacha aende ulikuwa ni uamuzi wa busara katika maisha yako.
.
Usihofu,utafika hatua hiyo.
😟😟😟😟😟😟😟😟😟😟
__,,,,____,,,,_,,,,,,____,,,,,,___,,,,,___,
Like
Share

Image may contain: 1 person


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/unaweza-kuwa-unaumia-sana-muda-huu.html

No comments:

Post a Comment