Thursday, March 26, 2020

Unajua ni Kwanini Wanawake wa Dar es Salaam Huibiwa Waume zao na Wafanyakazi wa Ndani?Sababu kuu Hii hapa


Fikiri hili, wewe ni mwanamke mrembo wa wastani, mwenye hofu ya Mungu. Kila siku jioni huwa unakwenda kufanya mazoezi baada ya shughuli za siku na hii hukufanya uchelewe kufika nyumbani mara kwa mara.
Una kazi nzuri na mshahara mzuri wenye tarakimu nyingi kama namba ya simu.  Umeona gari zuri na ukaamua kulinunu tena kwa fedha zako mwenyewe na Mungu akakujali kupata mume mtanashati na baraka ya watoto wawili.
Lakini kutokana na wingi wa majukumu unaona utafute dada wa kazi ambaye atakusaidia shughuli za nyumbani. Dada huyo unamtoa huko kijijini Sitimbi na wakati mwingine hata jina la ulipomtoa hukumbuki kwa jinsi lilivyogumu.
Mumeo, kama walivyo wanaume wengi wa mjini, wao huwa hawahusiki na kuchagua dada wa kazi. Lakini akija unamuuliza mumeo, umependa huyu dada wa kazi? unamiini atakuwa msaada kwetu.
Msichana huyu huyu uliemtoa huko kijijini pengine hajui kushika hata kalamu aandike jina lake. Pengine anamiliki mkoba wake mdogo aliotoka nao kijijini na sura yake ya kuvutia ambayo hajajua kuitunza lakini itaanza kuonekana akishaizoea nyumba.
Ili kumuonyesha wewe ndio mama mwenye nyumba, utakuwa ukigomba na kumuelekeza namna ya kuvaa hasa wakati baba nani hii yupo. Utaenda sokoni kumnunulia nguo ambazo zitamfanya onekane kama mzee. Hii ikiwa ni njia ya kutaka kumlinda mumeo asiangukie kwenye mtego.
Lakini wewe upo busy kuvaa sketi fupi na vinguo vya kuacha maungo wazi kuonyesha wewe ndio mwenye mamlaka katika nyumba. Kitu ambacho hujui ni kuwa huyu msichana wa kijijini  na yeye anajua namna ya kumpeti peti mwanaume kama wa mama wa vijijini.
Msichana atakuja wakati mumeo yupo sebuleni na kukunja goti kwa heshima akimuuliza kama anataka kuandaliwa maji ya kuoga. Sasa kwa mwanamke wa mjini hadi akunje goti labda wakati anatafuta remote ya Tv aangalie tamthiliya za kifilipino.
Mara ya mwisho mke wake kumuuliza kama anataka kuandaliwa maji ya kuoga, Tanzania ilikuwa chini ya mfumo wa chama kimoja. Mumeo atakunja gazeti lake, na kukubali  kuwa aandaliwe maji.
Dada wa kazi ataandaa maji na kuhakikisha yapo katika joto linalotakiwa, asijeunguza ngozi ya bosi wake. Wakati huo mke wa mtu anachati na marafiki zake kwenye mitandao ya kijamii bila kujua upande wa pili anampoteza mume.
Unaona kuwa ni vitu vidogo sana ambavyo wanawake huwa hawavifanyi na kuviacha kwa wasaidizi wao wa nyumbani wafanye kwa ajili ya waume zao bila kujua kuwa kwa kufanya hivyo wanajitengenezea njia ya kuwapoteza waume zao kwa dada wa kazi.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/unajua-ni-kwanini-wanawake-wa-dar-es.html

No comments:

Post a Comment