1:UHUSIANO WAKO BINAFSI NA MUNGU.
Uhusiano wako na Mungu hakikisha uko imara na unafanya juhudi za kuimarisha uhusiano wako na Mungu zaidi ya uhusiano wako na girlfriend wako.
Mwanaume anayempenda Mungu kwa moyo wake wote huyu lazima atampenda tu mke wake .
Maana atamsikiliza na kumtii Mungu,neno la Mungu limesema enyi waume #wapendeni wake zenu ,hivyo kwa sababu Mme anampenda Mungu automatically atampenda mke wake.
Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;(Waefeso 5:25)
a)Mme/kijana Usiwe mtu wa kukumbushwa kwenda kanisani.
b)Je unaomba mara ngapi kwa siku,kwa week unafunga mara ngapi kwaajili ya Maombi yako binafsi sio yale yanayotangazwa na kanisa au serikali.
c)Unampigia girlfriend wako simu mara kumi kwa siku,unaongea mara ngapi na Mungu kwa siku?
d)Unampa Girlfriend/mpenzi wako simu na zawadi za Garama ,sadaka unatoa shilingi ngapi jpili au kila unapoenda kwenye ibada?
2:NENO LA MUNGU
Hakikisha unalijua neno la Mungu na unaweza kumfundisha Mke wako unayetaka kumuoa.
Mwanaume alipewa neno la Mungu kwanza kabla ya kuletewa mke
Nia ya Mungu ni mwanaume alijue Neno,aliishi na aweze kulifundisha kwa mke wake na watoto wake.
Mme ni kichwa,mme ni kiongozi, mme ni Mwalimu.Familia inakutegemea uwafundishe na kuwapa mwongozo.
a)Je wewe unalijua neno la Mungu?
b)Unalisoma neno la Mungu mara ngapi kwa siku?
c)Je utaweza kumfundisha mke wako na watoto Neno?
Ukilijua neno la Mungu
d)Utampenda mke wako maana utalitii neno linalosema enyi waume wapendeni wake zenu.Hutampenda mke kumfurahisha bali utafanya kulitii neno la Mungu linalosema enyi waume wapendeni wake zenu
e)Ukilijua neno utaiogopa dhambi wewe binafsi na sio kwa kuambiwa na mchumba wako/mke wako.
Yaani wewe ndio umkanye mchumba wako juu ya kutofanya uzinzi kabla ya ndoa na sio uwe sababu ya kumfanya mzini kabla ya ndoa.
Mkumbuke Yusuph alikimbia na kumuachia kanzu Mke wa Potifa na kusema nimtendeje Mungu dhambi kubwa namna hii.
Swala la kuchepuka na kuwa na wanawake wa nje huwezi fanya kama unalijua neno kuwa uzinzi ni dhambi na Una Roho Mtakatifu ndani yako anayekukumbusha na kukuonya.
3:KAZI
Hakikisha una kazi inayoeleweka,panga mikakati jinsi gani utaweza kuitunza ndoa yako na familia.
Sifa ya Mwanaume na
Kiburi kiko katika uwezo wa yeye kuweza kuhudumia familia yake mahitaji yote ya Muhimu.
Kiburi kiko katika uwezo wa yeye kuweza kuhudumia familia yake mahitaji yote ya Muhimu.
Sasa rafiki yangu unataka mke je una kazi ambayo unajua huyo binti ukimuoa utaweza kumtunza na kumhudumia kila jambo,au ndio wale mnataka wake zenu ndio wawahudumie ninyi?
Utaweza kumpa chakula?,utaweza kumpa pesa aende saloon apendeze kama wanawake wengine?Unasehemu ya kumlaza?
Vijana wengine unakuta wanaoa lakini hawawezi kuwahudumia wake zao,wengine wanaoa wanawepeleka wake kukaa kwa wazazi wa mme,hii ni hatari sana
Maana ukitaka mkeo agombane na wazazi wako mpeleke akaishi nao nyumba moja na washare vitu,bifu lake lisikie tu.
Raha ya wakwe ukawatembelee na sio kuishi nao na kushinda nao aisee .
Mungu alimpa Adamu kazi kabla ya kumleta Eva.Hivyo kazi ni jambo la muhimu kwanza kabla ya mke.
Sio unaoa unategemea kulishwa na mke.
Wanaume/Vijana fanya kazi kwanza.
4:MAONO
Una maono gani,unajiona wapi miaka miwili,mitano ,kumi ijayo??
a)Je unalijua kusudi la kuumbwa kwako?
b)Unajua kuwa mke unayemuoa kazi yake ni kuja kukusaidia wewe kuliishi hilo kusudi?
c)Utakapooa na hujui kwa nini uliumbwa,huna maono wala ndoto zozote katika maisha sasa mke unataka aje kukusaidia nini,maana yeye ni msaidizi au unataka msaidiane kuzaa watoto๐๐๐
Tafadhali hakikisha una mambo hayo mambo manne kwanza
Tuendelee kesho
Pastor Winnie Kilemo
Pastor Winnie Kilemo
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/kijana-kabla-ya-kutaka-mke-hakikisha.html
No comments:
Post a Comment