Friday, March 27, 2020

WANAWAKE ACHENI KUDHARAU NDOA,NDOA NI MPANGO WA MUNGU.


Niujinga na upumbavu wa kiwango cha PHD kuanza kuiponda na kuidharau ndoa ya mwanamke mwenzio ili hali wewe hata pete ya uchumba hujavishwa hata huyo mchumba hajajitokeza na pengine huna hata mahusiano mema yenye malengo ya ndoa hapo baadae,na pia inawezekana kabisa pengine hata umri unakutupa mkono na hata kama umri wako bado je una fahamu utakuja kuolewa na nani au utakuja kuwa na ndoa ya aina gani?.
Kuyadharau mahusiao hususani ndoa ya mwenzio ni ushamba wa hali ya juu na inawezekana kabisa ukawa unajitengenezea msimu mbaya kwa mwenyezi Mungu,Ndoa na iheshimiwe na watu wote,wanawake acheni kuwa dharau wanawake wenzenu walio kwenye ndoa,cha msingi ni kujifunza kutoka kwao kuhusu ndoa ili uingiapo uweze kifanya vizuri zaidi.
Wakati mwingine una mlaumu Mungu kuwa hakupi ndoa wala hakupi mahusiano yenye malengo mema kwako,kumbe umesahau kuwa wewe ndio wa kwanza kuidharau mipango ya Mungu na kuiharibu,kumbuka Ndoa ni mpango wa Mungu kuidharau ni sawa na kumdharu mwenyezi Mungu na kujiondoa kwenye fungu la balaka juu yako,wanawake hususani mabinti badilikeni msidharau Ndoa za wenzenu.
Mbundason


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/wanawake-acheni-kudharau-ndoandoa-ni.html

No comments:

Post a Comment