Saturday, February 29, 2020

YAJUE MAMBO YANAYOUA MAHUSIANO NA NDOA NYINGI!


Image may contain: 2 people, people standing, shoes and outdoor
NDUGU.
JAMII.
MTOTO/WATOTO.
MARAFIKI.
WIVU WA KI MAENDELEO.
SIRI.
UBINAFSI.

Hawa ndiyo maadui nambari moja kwenye MAPENZI na kama unashiriki nao ni ngumu kuwa na mahusiano IMARA
Ndugu anabaki kuwa ndugu, Kwa vyovyote vile MAPENZI ni jambo binafsi otherwise wewe ndiye usababishe ndugu kuingilia Mahusiano/ndoa yako kitu ambacho ni hatari, NDUGU hajui radha na yote uyapatayo kwa mwenza wako sana sana anaweza kuwaka wivu akakuharibia kwa dhamana ya UNDUGU.
Jamii haiwezi kuwa sehemu ya FURAHA NA AMANI yako hivyo ni jikumu lako kuweka mipaka juu ya mtu kutaka kujua yaliyopo kwenye UHUSIANO/NDOA yako vinginevyo unaweza kusababishiwa aibu hata usiweze kutembea na mwenza wako kwa kuhisi WANAKUCHEKA.
Mahusiano/ndoa nyingi za sasa unakuta mtu tayari ana mtoto/watoto ambao alizaa na mtu mwingine kwa namna yoyote ile unaweza kujikuta unaona kama unamuonea/unawaonea watoto wako kwa kudhani uhusiano/ndoa uliyopo nje ya mzazi wao kwao ni ki kwazo kumbe ni ile hali ya ubin adam inayowapata watoto kwa kudhania Baba au Mama mpya hawezi kuwapenda kitu hicho kitawafanya kutompa UPENDO Mtu uliyenae, Mwisho kabisa utahisi Mtoto/watoto wako hawaupendi UHUSIANO/NDOA uliyopo, Na hapo taratibu PENZI LITAZAMA.
Marafiki hawa bwana ujue kila mmoja na mtazamo wake, Unaweza kupata Mtu wao wasimpende ama wakasikia wivu kwa namna unavyopendwa sasa usipokuwa makini wewe mwenyewe utajikuta huna msimamo mwisho kabisa kuhisi marafiki wanakuwazia mema mara moja utamuacha Mtu wako bila sababu.
Wivu wa kimaendeleo hapa napo panayo changamoto, Unajua Kuna watu hawapendi uwe na kitu kizuri kama hajakufanyia yeye na mara nyingi watu hawa ni wale WANAOPENDA Mtu asiendelee kwa kuhofia kumkosa Mwenza wake, Ni rahisi kuharibu uhusiano/ndoa ikiwa mwenzio atabaini hupendi maendeleo yake.
Siri ni nzuri lakini ujue kutofautisha yahusuyo siri, Kama unafanya uzinzi wewe ficha tu japo iko siku ufichayo yatakuwa wazi, Lakini kama unaficha mpaka mambo ambayo kwa uhalisia mwenza wako ni haki yake kuyajua Basi tambuwa kwamba kwa kuyabaini kwake bila wewe kusema NI NJIA RAHISI KWAKE KUANZA MASHAKA JUU YAKO na mara nyingi ukuta wa maelewano UTAJENGWA na mwisho kabisa ni migogoro isokwisha.
Ubinafsi ni SHETANI NAMBA MOJA KWENYE MAHUSIANO/NDOA YEYOTE hata kama uonyeshe upendo mkubwa namna gani mwenza wako akijuwa wewe ni mbinafsi ni rahisi kukutungia sheria kitu ambacho kitaleta vita ya ki MAENDELEO kwamba kwa sababu wewe vyako Mimi sipati Basi na vya kwangu sikupi, Mwisho kabisa ni kelele zisizo na mashiko.
Maana ya Mahusiano/ndoa na MAPENZI kwa ujumla wake ni mmoja kuunganisha nguvu zake na za mwingine na kujenga THAMANA YA KUWA WAMOJA kwa namna yoyote Wawili hao wanawajibika kila mmoja KUJUWA THAMANI YA MWENZA WAKE NA KUMTHAMINI hapo utakomboa uhusiano/ndoa yako kwa urahisi kabisa, Fikiria zaidi kuwa WAZI kwa Mwenza wako itakufanya hayo yote ambayo ndiyo chanzo cha mmomonyoko wa PENZI LAKO kutokuwepoπŸ’ͺ
Unapoingia kwenye MAHUSIANO/NDOA hayo mambo yakemee na Uweke ukuta yasiingie kwako ili ulifanye Penzi lako kuwa IMARA na hapo Mito ya FURAHA NA AMANI itakufuataπŸ’ƒπŸ’ƒ
Sasa ujifanye RUTHU ushakuwa na Mahusiano/Ndoa halafu kutwa kugeuka nyuma kuwatazama ndugu, jamii, marafiki, wanasema nini ITAKULA KWAKOπŸ˜…
Mwisho wao kabisa mchana lakini ukienda KULALA wewe ndiye utakosa usingizi wao watakuwa wanakoromaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Ukiambiwa ya watu changanya na yako ila lililo la THAMANI sikiliza MOYO UNATAKA NINI na hapo utachagua njia ikupelekayo kwenye AMANI yako😎
Mama wa yote Haya MSIMAMOπŸ’ͺ
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria πŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/yajue-mambo-yanayoua-mahusiano-na-ndoa.html

Ni rahisi kusahau maumivu ya kidonda, Lakini ni ngumu kulifuta kovu,

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Kweli kabisa ni rahisi kusahau maumivu ya kidonda, Lakini ni ngumu kulifuta kovu, Maana yake kovu ndiyo litakukumbusha chanzo cha maumivu uliyopitia wakati unaumia😭😭
UTAMKIE MOYO WAKO;
"Moyo wangu kuwa na SUBRA kila jambo huja kusababisha kujua na kujifunza, Lakini unapojifunza tengeneza njia sahihi ya kujua madhaifu yako mwenyewe yaliyopelekea kupata MAUMIVU"
Pengine ni UDHAIFU.
Pengine ni KUPENDA KUPITILIZA.
Pengine ni UWAZI ULIOPITILIZA.
Pengine ni NAMNA ULIVYO MHESHIMU.
Maana Kuna watu wengine ukimpenda sana huhisi kero, Lakini ikiwa wewe umewajibika ipasavyo kulilinda penzi lako na huoni kama unaeleweka LET GO
Huwezi kulifufua penzi lililokufa sana sana utajivika UTUMWA na mwisho kabisa uje kujutia muda uliopoteza😭😭
Kuna mtu unapokuwa muwazi yeye anachukulia kama tatizo, Kuna mtu unapokuwa mdhaifu kwake yeye anachukulia kama fimbo kukuchapia, Kuna mwingine ukimheshimu sana anaona huna pa kwenda, Ni wapumbavu pekee ndiyo huishi na akili za kijinga kiasi hicho, LOVE IS LOVE banaa, Ukipendwa unajisikia upo DUNIANI lakini ukose wa kukupenda Mbona MARADHI YOTE SUGU YATAKUPATAπŸ˜…πŸ˜…
Usimlazimishe Mtu awe nawe na ameona muda wako kwake umekwisha Nakusihi sana usijaribu kwa sababu bin adam wana tabia mbaya ya kuficha uhalisia na ndani yao wana mambo ya siri wala huwezi kujua, Mtu asiyekupenda atajitahidi kukujengea UONGO ambao utakufanya umpende na kumbe anae AMPENDAYE KWA DHATI ukija kushituka ULIISHAMPENDA lakini ndo hivyo tena kuna ambaye YUPO MOYONI MWAKE inauma sana, Kuna mijitu lina Mume/Mke kila siku kumponda ili likupe TUMAINI kumbe linaumizwa kule ndani linataka FARAJA KWAKO baadaye wakiisha ridhiana UTAKUWA FALA TU😭😭
Jifunze kuwa na Mtu wako Mwenyewe ambaye anatokana na NAFSI maana Kuna wakati tunahadaika na Macho, Moyo nao ni mdhaifu unadanganyika mwisho kabisa NI NAFSI KUHANGAIKA.
#Elista_Kasema_ila_Sio_SheriaπŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/ni-rahisi-kusahau-maumivu-ya-kidonda.html

UNAFIKIRI NI KWA NINI WANAWAKE NDIYO WAHANGA WA MAHUSIANO/NDOA KULIKO WANAUME?

Image may contain: 2 people, people smiling, people sitting
Wanawake mahitaji yenu ni Mengi juu ya Mwanaume, Wewe unataka;
UPENDO.
CARE.
ATENTION.
MUDA.
FAMILIA WATOTO.
MAISHA KWA UJUMLA.
Wakati mwanaume hitaji lake kwa Mwanamke ni moja tu nalo ni;
"STAREHE YA MWILI WAKE maana ameumbiwa TAMAA yaani kwake asipokuwa AMETAMANI anajiona kama DUNIA IMEMTUPA"
Sana sana akivuka kwenye HAJA YA MWILI pengine Mwanamke unacho kinacho Mvutia kuwa nawe, Vinginevyo ukiisha MVULIA NGUO NA AKAPATA HAJA YAKE kuendelea ni BAHATI.
Ndo Maana napenda kuwaasa Wanawake mjifunze kusitahamili MAHITAJI YENU ili iwe ngumu kwa Mwanaume KUKUTUMIA KAMA CHOMBO.
Uliishaumizwa mara ya kwanza usiondoke kwa kujipa MOYO kwamba pengine huyo alikutamani tu, Fikiria zaidi ni kwanini ALIKUACHA? Kwa sababu unaondoka kwa Mwanaume na unakwenda kwa Mwanaume hivyo unatakiwa kuwa MAKINI japo kujichunguza na kujua kama wewe ni chanzo Basi uchukuwe hatua katika kukabiliana na changamoto za ki mazingira ya MAHUSIANO/NDOA Kwa mapana yake akili yako ifikirie zaidi KESHO kuliko leo ambayo tayari umeijuwa na kukabiliana nayo vinginevyo HUWEZI KUMPATA MKWELI KWAKO Kwani pengine wewe unamsababisha Mtu kukuona huna malengo nae kwa vyovyote vile atakulipa Sawa na unavyomchukulia.
Mwanamke na Mwanaume kinachowapa vita kwenye UHUSIANO/NDOA yao ni kidogo sana ila ndicho ambacho wengi hawakijui, Na badala yake wanabaki kuhisi HAWAPENDWI;
Mwanamke anataka Mwanaume awe MUME ili aweze kukabiliana na majukumu yake, Maana yake abadilike kutoka kwenye ujana na kuwa Mtu mzima, Ajue kwamba TAYARI ANAYO FAMILIA.
Mwanaume anapokutana na Mwanamke hupendelea zaidi ule utii wa Mwanamke na mara nyingi wanaume huuchukulia kama udhaifu, Na hapo Mwanaume atataka Mwanamke wake asibadilike, Na akibadilika ndipo MWANAUME HUHISI ANADHATAULIWA.
Hapo ndipo WAWILI hawa kushindwa kuendana na wasipokuwa makini MAHUSIANO ama NDOA waliyopo haiwezi kuwa IMARA zaidi ITAZAMA.
Ili kumlinda MWENZA wako huna budi kutambuwa MAHALA NA NAFASI ULIYOPO vinginevyo huwezi kumuona wa kukufaa Maana bin adam wote sawa, Na kwa Maana hiyo Basi ujue wazi NI NADRA KUMPATA AMBAYE ATAENDANA NA UTAKAVYO otherwise utumie nguvu za ziada kumuweka awe kama utakavyo.
#Elista_Kasema_ila_Sio_SheriaπŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/unafikiri-ni-kwa-nini-wanawake-ndiyo.html

UATESWA NA MAPENZI HEBU SOMA HAPA

Image may contain: 1 person, standing, close-up and outdoor

Huwezi kuyabadirisha yaliyokuumiza, Bali kupitia hayo unaweza kujivika ujasili kuendelea mbele hata kuufanya MOYO wako kurejewa na AMANI yake binafsi, Muda mwingine hatujui kwamba AMANI INATOKANA NA WEWE MWENYEWE kwa kushindwa kuweka uwiano baina ya HITAJI NA UHALISIA.
Unampenda mtu lakini yeye yupo kwako kwa mahitaji yake kamwe hamuwezi kusonga mbele, Unamhitaji Mtu kwa sababu zako lakini yeye anakupenda kwa vyovyote vile mtaishia kwenye ugomvi😭😭
Kwanza kabisa Kuna swali ni muhimu kujiuliza kabla hujawa tayari kumpa mtu nafasi;
"NINAMTAKA MTU WA AINA GANI?"
Kuna wakati unakutana na ambaye inawalazimu muwe wapenzi ila HAMPENDANI kutokana na UKARIBU pamoja na vile mtaonyeshana KUHITAJIANA mnajikuta mmezama penzini, Kumbuka huyo sio wa CHAGUO LAKO ila amepatikana kutokana na mazingira, Mlikuwa safarini ama ki kazi na wengine kampani ya marafiki inasababisha, Mwisho kabisa wa UHUSIANO huu ni pale atakapokuja MWENYE MAMLAKA KWENYE NAFSI YAKO hapo ndipo utajikuta njia pandaπŸ˜…πŸ˜…
Uhusiano hata uwe mdogo kiasi gani kamwe ALAMA HUWA HAIFUTIKI kwa udogo wake Kuna jema ambalo litakufanya kulikosa kwa ambaye yeye ndiye unamuona sahihi kwako, Jambo moja nawasihi ni kujaribu KUYAKWEPA MAHUSIANO YANAYOTOKANA NA BAHATI MBAYA hayo yana gharama kubwa sanaa, Ili uishi kwa kuilinda AMANI YAKO BINAFSI unatakiwa kujuwa hitaji lako na kulipa kipaumbele na kwa kufanya hivyo utakuwa UMEIKOMBOA NAFSI YAKOπŸ’ͺ
Yaliyopita yaache yawe kama fundisho, Anza upya japo ni ngumu lakini tambuwa kwamba;
KUANZA NI GHARAMA LAKINI UKIISHA ANZA UTATENGENEZA NJIA KUSAHAU YALIYOPITA NA KUBAKI KAMA SIMULIZI.
Gharama ya Maumivu ya MAHUSIANO inajengwa tangu mnapokutana, Yaani ule Mwanzo ndiyo unaoweza kuleta TASWIRA ya Mwisho wenu, Kuna wakati unahisi mambo hayaendi vyema ila ukajipa TUMAINI atabadilika hapo ndipo UNACHOCHEA MOTOπŸ”₯
Akibadilika MSHUKURU MUNGU ila kama itakuwa ndo mwendelezo wake wa kukupeleka KWENYE MAUMIVU rafiki huwezi kubaki salama
Inuka ujitetee binafsi yako ili ile AMANI itokanayo na wewe Mwenyewe iweze kufanya Kazi ili kukulindia MOYO WAKO.
#Elista_Kasema_ila_Sio_sheriaπŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/uateswa-na-mapenzi-hebu-soma-hapa.html

KUNA TOFAUTI KATI YA KUTESWA KWENYE MAHUSIANO NA KUJITESA KWENYE MAHUSIANO!


(1) Hujawahi kumfumania mwenza wako lakini kila siku una kazi ya kukagua simu yake ili kutafuta kama anachepuka au la! Hukuti kitu lakini kesho yake bado unahangaika basi wewe jua tu unajitasa kwenye mahusiano na kama una hii tabia jua tu kuwa hata ukimfumania, narudia hata ukimfumania hapo anafanya huwezi kumuacha! Yaani kama wewe ni mtu wa kukagua simu kutwa mara tatu, awe ni mume, mke, mpenzi au nani basi huna ujasiri wa kumuacha, ni sawa na Mbwa kukimbiza gari, hainamaana anajichichosha tu kwani hata akilikamata hawezi kuliendesha hivyo acha kujichosha.
(2) Kumfuatilia kila mtu anayeongea na mpenzi wako; Unayafanya mahusiano yako au ndoa yako kuwa kama mahakama, kwamba mwenza wako kila dakika anatakiw akujielezea kwako, anaongea na mfanyakazi mwenzake basi anatembea naye,k kuna mtu kamsalimia labda wewe kakupita basi anatembea naye, kuna mtu kamchekea basi unauliza ni nani na anatembea naye! aina hii ya mahusiano inaboa na mara nyingi mtu akichoka unakuta ushaachwa bila kujijua kwani mtu anajiona kama yuko mahakamani anatakiwa tu kujitetea kila dakika!
(3) Wale watu ambao kila kitu wanahisi wanadharauliwa; Hawa ndiyo wanajichosha na kujinyanyasa mpaka basi, mtu kachelewa kupokea simu ushaanza ananidharau kwakua sina kazi,a nadharau kwakua kwao wanapesa, anadharau kwakua hivi vile, yaani mtu kashaaua kitu ulichomuambia jana yake unahisi unadharaulika, mtu kakose akidogo unahisi nikwakau kakudharaau, simu imekatika bahati mbaya au amekuambia yuko bize, hajajibu meseji yako wewe ni kudharaulika mpaka basio, unalazimisha udharaulike, ukijiona hivi basi jua kuwa hunyanyaswi bali unajinyanyasa!
Kama una tabia hizi za kujitesa basi jua kuwa mwenza wako hata akupe dunia bado hutaamini, hicho uanchokilalamikia kila siku akikupa utatafuta kingine. Inawezekana kweli mwenza wako ni msheniz lakini kinachjokuumiza si ushenzi wake bali kwakua huna amani ya nafsi. Amua leo, najua ngumu lakini amua kubadilika, hembu sema kuwa sitaki kitu flani naacha kitu flani. Utaona kuwa unabadilika unakua na furaha na mwenza wako naye anakufurahia. Jifunze namna ya kujipa furaha yako mwenyewe, soma kitabu cha “ndoa Yangu Furaha Yangu” Se4hemu ya nne, naa cha kujitesa mwenyewe huku ukisingizia unateswa.
idd makengo


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kuna-tofauti-kati-ya-kuteswa-kwenye.html

HIVI UNAJUA HUU NAO NI UTUMWA MWA MAPENZI

Image may contain: 1 person, sitting, table, drink and indoor

Ukitaka kuwa MTUMWA ama MHANGA wa MAPENZI Basi wewe jitutumue kwa dhiki zako ukaanzishe UHUSIANO na Mke/Mume wa mtu, Wala huhitaji kubet ni nini kitatokea baada ya kuwa ushaingia penzi hilo bali wewe TARAJIA MAUMIVU TU.
Mara nyingi Mke/Mume wa mtu anapoanzisha uhusiano nje ya NDOA yake maana yake yeye amedhamiria kujifurahisha ama kwa lugha rahisi;
KU-REDUCE STRESS ZA NDOA YAKE.
Wakati huo huo ujue NDOA ipo na Kuna wengine na kule ndani anatumika ki mwili kama kawaidaπŸ˜…πŸ˜…
Hakuna Mtu mbaya kwenye Swala la radha kama MPISHI ndo maana ukikuta MPISHI ni mwembamba ujue MCHOYO ila nature ya kazi ya UPISHI ni kuonja kwingi na KUNENEPEANAπŸ˜…πŸ˜…
Mume au Mke wa Mtu aliyetoka kwenye NDOA yake na kuanzisha MAHUSIANO NJE ni kama MPISHI Yaani kwake hata aonje mara ngapi lakini kila anachopika lazima aonje tu ili kuhakiki radha inayotokana na chakula husika.
Mwana ndoa yeyote akiishaanza USALITI kamwe hawezi kuacha, Kwa sababu moja tu;
ALIISHAJUWA YA NDANI HAIWI TAMU KAMA YA KUIBA HIVYO HUWEZI KUMTENGA NA KUCHEPUKA HATA UKIMBANA VIPI AKIONA MUDA NA NAFASI NI NDOGO HATA KIJAKAZI WAKE AWEZA KUMPATIA.
Mbadala wa kutofurahia ndoa ni KUACHANA wala sio kuonja onja huko mabarabarani maana mwisho kabisa ni kujiweka kwenye HATARI.
Mke wa Mtu ama Mume wa Mtu kamwe hawezi kujenga UHUSIANO WA KUDUMU japo anaweza kudumu yeye kwa sababu zake ila sio kumfanya DOWEZI kufurahia, Mara nyingi wanaachaga vibaya sana na Kuna wengine ni wajinga NDOA ANAITAKA NA MCHEPUKO ANAUTAKA mwisho kabisa NDOA inabaki na nafasi yake kwa sababu tayari ni NDOA sasa huko nje ndipo kinapowaka motoπŸ”₯
Kwa sababu ukiwa MWIZI WA MKE/MUME wa Mtu utajengewa kujiona wewe ni zaidi ya MWENYE NDOA YAKE kumbe si lolote wala chochote, Wewe ni MSAGA SUMU TU mwenzio anajua atakalo kwako, Ni bora kukosa UHUSIANO kuliko kutembea na MKE au MUME wa Mtu hao ni NYOKA🐍
Yaani siku akikutemea sumu yake RAFIKI WAFWAAAAA😭😭😭
Ya nini kutaka kero kwa mtu ambaye unajua kabisa MWISHO UPO? Kwa sababu tayari anae wa kwake, Kama unao UGWADU na umempenda basi usiingie kwake kwa MTAZAMO WA UPENDO bali ingia na TAMAA ZAKO nenda kupumue ukimaliza sepa ila ukinogewa USIJENGE MZINGAπŸ˜…πŸ˜…
Mume au Mke wa Mtu ni watu waongo na walaghai sana, Hakuna hata mmoja atamsifia mwenza wake ili wewe ujione Uko SPECIAL kumbe mwenzio anatafuta Kivuli na akiisha ona Mvua ama Jua kuzama anatazama NDOA YAKE mtu wa aina hiyo hata iwe na INSTRUMENTAL🎹 fanya kama hujui maana ya mziki ili usije kuumia, Raha ya MAPENZI uwe na Mtu ambaye utakuwa nae HURU pamoja na kujivunia uwepo wake kwako, Penzi lenyewe la siri INAHUSU?
Kuna Mijitu Mingine ni vichwa maji unakuta NDOA imelitesa balaaa, Unalipa TRUE LOVE lakini wala halioni kisa KABILA AMA DINI likakupa STRESS zisizo na Maana, Ukiona ni Mke ama Mume wa Mtu TUMIA AKILI KU-DEAL na Mtu wa aina hiyo, Vinginevyo WEWE NDO UTAKUJA KUJUTIA😭😭
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria πŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/hivi-unajua-huu-nao-ni-utumwa-mwa.html

PENZI KUWA BORA AU BOVU INATEGEMEA NA ULIANZANJE.

Image may contain: 2 people, outdoor

Kuutunza MWANZO ni GHARAMA lakini FAIDA yake ni ADHIMU.

Kama kuna kitu kigumu japo kina manufaa ni KUUTUNZA MWANZO WA PENZI yaani ile TASWIRA ambayo iliwafanya wawili KUPENDANA hiyo ndiyo yenye MAANA ZAIDI kuliko hata UPENDO WENYEWE.
Kwa sababu UPENDO NI TENDO LA NAFSI na kwa vyovyote vile ni ngumu kujuwa kwa hakika ikiwa Mtu anamaanisha asemacho, lakini MATENDO YANALETA MAANA HALISI YA UJUMBE WA NAFSI kuliko MANENO.
Uzembe huanzia kwenye KUJISAHAU na mwisho kabisa UANGAMIVU HUINUKA KWA KUJIAMINI hapa ndipo Mtu anaweza KUMPOTEZA MTU WA MUHIMU kwa kushindwa kutambuwa kwamba;
"PENZI NI MFANO WA BUSTANI KWAMBA KILA SIKU LAZIMA UNYESHEE MAJI🚿" Unapoona PENZI LAKO LIMECHANUA🌷 ukajisahau na kujiamini niamini UKAME UTALIKUMBA PENZI LAKO na mwisho kabisa ni wewe kuingia kwenye MAUMIVU. Uliyoyatarajia YANAWEZA KUJA IKIWA UTAJUWA KUYALINDA lakini ambayo HUKUYATARAJIA HUJA KWA UJINGA WAKO MWENYEWE.
Utunze Mwanzo wa penzi lako ili ujiweke kwenye AMANI YA MOYO WAKO maana hilo ndilo chaguo lako, Lakini ukiona nakufundisha sana fanya kama hujaelewa namaanisha nini ili uje kujutiaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
#Elista_Kasema_ila_Sio_SheriaπŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/penzi-kuwa-bora-au-bovu-inategemea-na.html

Friday, February 28, 2020

DOWNLOAD APP BORA YA VICHEKESHOO HAPA



source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/download-app-bora-ya-vichekeshoo-hapa.html

MWANAMKE USISHINDANE NA MWANAUME KWA KUJIONA UNAWEZA⛔


Image may contain: 2 people, people sitting
Wanawake wengi wamejikuta wanazama kwenye MAUMIVU MAKALI bila kujua chanzo, Nimebaini kwamba WANAWAKE wengi wamejikuta wanaolewa na wanaume ambao hawakuwatarajia ila ni kutokana na WALIOWATARAJIA KUTOONYESHA KWAMBA WATAKUWA WENZA WAO.
Pamoja na UVUMILIVU wa Mwanamke kusubiri pengine kungetokea mabadiliko lakini haikuwa pengine kwa wakati ama kwa sababu, Na Mwanamke kukata tamaa ya kuendelea hata akajinasibu kutafuta Mtu mwingine ambaye yeye Mwanamke ataweka sharti la NDOA na kwakuwa Mwanaume ni kama PANYA hachagui kichaka anajikuta AMEJITWALIA MKE bila kutarajia, Wakati huo huo Mwanamke anajikuta ameolewa na Mtu ambaye hakuwa ndiye chaguo lake, Mwisho kabisa wa NDOA HIYO NI MASIMANGO😭
Kila mmoja akitamba ki vyake lakini ambaye itamgharimu ni MWANAMKE kwa sababu unakuwa na aina mbili ya MAUMIVU;
 KUMKOSA ALIYEMPENDA.
 KUDUMU KATIKA NDOA NA MTU AMBAYE HAKUMPENDA.
Moto wake uwakao MOYONI ni dhahiri HUWEZI KUSALIMIKA
Shauku ya NDOA imewagharimu wengi, Kwamba Mtu aliweza kuwa kwenye MAHUSIANO miaka 3 alifurahia sana MAPENZI Lakini alipomkosa aliyempenda na kuolewa/kuoa Mtu mwingine wiki moja kwenye ndoa hiyo ni Sawa na MIAKA KUMI Yaani kila kunapokucha wazo kuu ni namna gani nitachomokaπŸ˜…
Kusubiri kunawapasa wenye MIOYO YA UVUMILIVU na hao mara nyingi hushinda mitihani yoteπŸ’ͺ
Wanawake punguzeni kuyapenda MAGAUNI YA HARUSIπŸ‘— wala msipende chereko chereko za marafiki pamoja na ndugu, Hao wanabaki kuwa MASHUHUDA TU na wala hawataingia kwenye kukusaidia wakati wa MATESO YAKO KWENYE NDOA ambayo hukuitarajia, Balaa kubwa ni pale unapoanza kuishi na Mtu ambaye hukumtarajia kwa kifungo cha NDOA niamini pamoja na kutomtarajia lakini Kuna kitu kitakugharimu kuachana nae MAZOEA.
Mazoea yanajengwa na UKARIBU hata kama hamko kwenye GOOD TERMS lakini unaweza kujikuta HUTAMANI KUACHANA NAE wakati huo huo huhisi KUMPENDA πŸ˜… na hapo ndipo utajikuta njia panda mara na ka mimba kamepenya weeee utabakia kuwa MHANGA wala usijue MBIVU ni zipi na MBICHI ni zipi? Uonapo uliyempenda Bado hajawa tayari kwa utakayo jipe muda kuendana nae ili usije jikuta UMEMUACHA kwa kujiamini kwamba utampata mwingine kwa MASHARTI yako niamini UTADUMU KWENYE UNYONGE.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria πŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwanamke-usishindane-na-mwanaume-kwa.html

UKITAKA KUFURAHIA NA KUIONA AMANI KWENYE NDOA YAKO BASI HUNA BUDI KUFANYA HIVI

Image may contain: 1 person, smiling, outdoor

Mwanaume umuoe Mwanamke ambaye umemzidi Umri, Elimu, Pamoja na kipato ili ile hali ya UTII WA MWANAMKE ukadumu MAISHANI mwako ikiwa utajitenga na unyanyasaji kwa Mkeo na ukatawaliwa na HEKIMA.
Mwanamke uolewe na Mwanaume kwa UTASHI wake, Uwe na umri chini yake, Wala usilazimishe kuwa na kiwango Kikubwa cha Elimu zidi ya Mumeo pamoja na kusimama kwenye eneo lako kama MAMA itakupa kuepuka KUJIHESABIA HAKI na kumuona Mumeo ni Mtu tu.

Kwanza Wanawake wote mjue ujanja wenu ni kwenye USICHANA Yaani kabla hujazaa ila ukiishaitwa MAMA rafiki yangu kama hujajitambuwa MAISHA YAKO BAADA YA KUMKOSA ALIYEKUZALISHA AMA MZAZI MWENZIO ni sawa na Mpira wa kona Yaani kila mmoja anataka kuugusa😭😭
NDOA za namna hiyo nimeisema kwenye kichwa cha ujumbe wangu wengi wamedumu na kushiriki HESHIMA YA UPENDO kwa sababu Mume awapo kwenye kiwango cha hayo nilosema ni nadra Mwanamke kutomtii Mumewe, Lakini pia Mwanamke akiwa eneo lake nililolisema ni ngumu kwa Mwanaume kuhisi DHARAU kwa mkewe, Wanawake wengi mkisoma ama kuwa na hakika ya vijisenti mnataka kuwapanda vichwani waume zenu, Huku mkisahau akina BETINA wale wadangaji soko lao kuu WAUME ZA WATU wanaotaka FARAJA
Ndoa ni eneo TAKATIFU SANA japo wengi wamelifanya kama HAKIKA YA MATUMIZI YA MWILI kumbe ni HEKALU LA MUNGU.
Ili kuwa na NDOA IMARA kila Mtu na ajichunguze nafasi aliyopo na akatae ULINGANIFU
Mwanamke mkatae Mume age yako, mishahara inalingana, Level moja ya Elimu Huko ndani mnakwenda kutengeneza BOMU likilipuka MWAFAAAπŸ˜…
Mwanaume vivyo hivyo, Na kwako ni lazima uoe Mtu aliye chini yako ili kuweka HESHIMA KWENYE MAISHA YENU ile hali ya UFALME iwepo kwa wewe kumhudumia Mkeo na familia kwa ujumla vinginevyo UTAJUTIA.
Mwanaume DALALI huna Elimu, Mkeo ana PhD unategemea Kuna UTII utauona hapo? Ukiwaangalia wenye MAFANIKIO Kwenye NDOA zao unakuta BABA PROFESSOR na Mama Mwalimu wa msingi hapo UTII KAMA WOTEπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒ
Lakini pia niwakumbushe wanawake wote mnaotaka wanaume walio chini yenu ili kuwatawala MWANAUME NI MWANAUME BY NATURE anataka utii wako kwake, Kwa ujinga wake UTADUMU NAE ila mwenye akili itakuwa kama KUMPIGA TEKE CHURA eneo yalipo Maji atapendwa na Marafiki zako, Ndugu zako mwisho kabisa ATAKUACHA UKILIA kwa sababu wewe hukumtii.
Fuatilia ndoa za KUKURUPUKA ZINAVYOWATESA WENGI kila kukicha wakitafuta njia ya kuchomoka wala wasiweze, Ukiingia NDOANI umejinasisha mwenyewe UPAMBANE MPAKA KIELEWEKEπŸ˜…
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria πŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/ukitaka-kufurahia-na-kuiona-amani_29.html

MBINU ZA KUMWOMBA MSAMAHA MPENZI WAKO



Marafiki zangu kukosea katika maisha ya binadamu ni kawaida. Ni sehemu ya maisha yake. Tena inaaminika kwamba, kukosea ni kujifunza, maana kosa utakalofanya leo ni funzo la kesho. Hii ipo pia hata katika uhusiano na wapenzi wetu, mara kadha wa kadha tumejikwaa na kuwakosea.

Hakuna cha ajabu. Ni kawaida kabisa, lakini jambo la msingi hapo ni kwa namna gani tunajifunza kupitia makosa. Ni kwa jinsi gani tunamaliza tofauti hizo. Maana unaweza kuwa hodari wa kukosea au ukawa bingwa wa kusamehe, lakini wimbo huo ukaendelea kubaki hivyo hivyo kila siku.
Lakini pia, wapo ambao kwa bahati mbaya, bila matarajio yao, wanajikuta wakiwa wamewaudhi wapenzi wao. Ni bahati mbaya na yawezekana kabisa wanaumia sana mioyoni mwao, lakini wakashindwa jinsi ya kumaliza ‘bifu’ hilo katika penzi lake.
Siku zote mkosewa hukosa raha, hupoteza hamu ya kukutana na mpenzi wake lakini kubwa zaidi, hujishusha/hukushusha thamani ya mapenzi yake kwako. Lakini mkosewa huyo huyo, akioneshwa kwamba makosa yaliyofanyika hayakuwa ya makusudi na kutumia njia bora za kufikisha hisia zako kwake, hujisikia amani na hali yake kurejea kawaida.
Rafiki zangu, yawezekana ukawa upo katika kipindi cha matatizo na mpenzi wako na hujui jinsi ya kuweka mambo sawa. Wakati mwingine huna tatizo, lakini kwasababu upo kwenye uhusiano basi si ajabu mambo kwenda mrama siku moja.
Hapa chini, nimekuandalia mambo matano muhimu ya kuzingatia unapokuwa umekwenda kinyume kidogo kwa mpenzi wako. Weka ubongo wako wazi, kuruhusu somo hili kichwani mwako, ambalo litakuwa hazina yako na mwongozo katika uhusiano wako.
KOSA LINA UKUBWA GANI?
Hapa tayari umeshagundua kwamba umemkosea mpenzi wako na ni kweli kwamba unaumizwa sana na kosa lako, lakini kwasababu hujamwambia chochote, naye hana raha na wewe. Hana amani ya moyo.
Hapa unashauriwa kutulia na kutafakari ukubwa wa tatizo. Kufahamu ukubwa wa tatizo kutakupa muongozo mzuri sana wa jinsi ya kutatua tatizo hilo. Angalia ulimfanyia nini na kwa kiwango gani?
Mathalani unaweza kuwa ulimuudhi kwasababu alikupigia simu zaidi ya mara kumi bila kupokea, akakasirika. Hili ni kosa dogo.
Lakini yawezekana alikuta sms ya mapenzi kwenye simu yako au alikufumania; haya ni makosa makubwa. Tafakari na ujue ukubwa wa kosa lako.
ONESHA UNAVYOJUTA
Hii ni kwa ajili yako wewe mwenyewe. Rafiki zangu, kutakuwa hakuna maana yoyote kuomba msamaha wa kinafiki au kuomba msamaha ili kumaliza mambo, kama msamaha wako haujatoka moyoni.
Ukiwa peke yako, jiaminishe kwamba umekosea na kwa hakika unahitaji kusamehewa. Jutia ndani ya moyo wako, kwa dhati kabisa ukiwa na ahadi kwamba hutarudia tena. Hili ni zoezi la Kisaikolojia, ambalo litakusaidia baadaye wakati ukikutana na mpenzi wako kwa ajili ya kuomba msamaha.


KUWA MKWELI
Omba kukutana naye. Yawezekana hata mawasiliano si mazuri sana, lakini hapa jitahidi kumuomba mkutane, ikishindikana, tumia mtu wa karibu sana na yeye. Omba kutoka naye kwa ajili ya kuzungumza.
Mweleze ukweli wa kosa lako, onesha jinsi linavyokutesa na kukusumbua. Usijaribu kuongea uongo wowote katika suala hili. Kuwa mkweli. Jutia kwa moyo, aone majuto yako usoni mwako.

Mwambie jinsi unavyoteseka na jinsi msivyo katika maelewano mazuri. Kauli yako ya ukweli, hisia zako wakati wa kuzungumza, ndivyo vitakavyokuweka katika mazingira mazuri ya kuweka mambo sawa.

MHAKIKISHIE HUTARUDIA
Bila shaka, kama utakuwa umefuata taratibu zote hizo kwa umakini, uwezekano wa kusamehewa ni mkubwa sana. Hili ndiyo matarajio yangu, naamini hata wewe pia, lakini ili msamaha huo ukamilike, mhakikishie mpenzi wako kuwa hutarudia tena.

Mwambie kwa kumaanisha, kwamba umegundua udhaifu wako na haupo tayari kumfanya tena asiwe na furaha tena. Hakuna uchawi ni maneno tu!

FANYA KITU MAALUM
Hapa unatakiwa kufanya kitu maalumu kwa ajili ya mpenzi, ukionesha kwamba umekubaliana na msamaha wake na mambo yameisha. Kitu utakachokifanya hapa utalinganisha na ukubwa wa kosa kama nilivyosema awali.

Mathalani unaweza kutoka naye na kwenda kulala naye hotelini, ukihakikisha unampa mahaba mazito kama shukrani kwake. Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya kulingana na uwezo wako kifedha. Fanya vyovyote ili kosa lile lisahaulike moja kwa moja!

Nimeeleweka? Ahsanteni sana marafiki zangu, hadi wiki ijayo tena kwa mada nyigine nzuri zaidi itakayokupa mwanga mpya katika maisha yako ya kimapenzi.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mbinu-za-kumwomba-msamaha-mpenzi-wako.html

Kwa wanawake tu; Fanya haya kumchizisha Mpenzi wako kitandani

Image result for walembo wa tanzania
Mtaalam wa mapenzi, Bi. Layla Quinn, anasema wamaume ni viumbe rahisi sana kuridhishwa tunapokuja katika suala la unyumba. Mwanzoni, kitu kinachomhamasisha mwanaume kujamiiana ni muonekano wako (mwanamke) tu wakimahaba, lakini kadri siku zinavyokwenda ndani ya mahusiano, inakuwa ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo barabara!
Bi. Layla anaendelea kusema kuwa, kumridhisha mwanaume wako kitandani inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya mvuto ( Remember to keep things intereting!). Tafuta namna ya kuleta hamasa, iliyokuwepo siku za mwanzo mwanzo, na kwa hakika utakamata usukani. Sasa swali linakuja…..Nini unatakiwa kufanya, ili kumridhisha mwanaume wako kitandani? Kujibu swali hilo, Bi. Layla amekuja na sheria 10 zifuatazo, ambazo kama zitazingatiwa kwa makini, basi mwanamke hatokuwa na shida ya kumridhisha mwanaume wake kitandani na nyanja nyingine muhimu za mahaba.
# 1 Vaa vizuri. Utamu wa kujamiiana unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe, lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine mengi. Vaa vizuri wakati wa kulala wakati wote, na sio tu wakati wa usiku, ambao unataka kufanya mapenzi. Vaa nguo nyororo, yenye mtelezo unaomwagika mwilini. Kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani, mwanaume wako hatotaka kutoa mikono yake mwilini mwako.
#2 Usiwe mtu wa aibu aibu linapokuja suala la kujamiiana. Mwaume anaweza akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni “innocence”), lakini hamna mwanaume atakaye endelea kuvumilia mwanamke, ambaye anastushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya kujamiiana), isipokuwa mtindo wa kifudi fudi, maarufu kama “Kifo cha Mende”. Wanaume wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kitandani. Wanaume wanapenda wanawake, ambao wanajiamini na wanabuni manjonjo mbalimbali wakati wa shughuli. Kama unataka kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi soma mbinu mbalimbali, ambazo zinatumiwa na wapenzi mbalimbali.
#3 Fanya mazoezi na onekana Bomba. Wanaume ni watu wakujali sana muonekano wa mwanamke. Kwahiyo, sio lazima kuonekana kama walimbwende wa vichupi, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi kitandani. Ndio, mwanaume wako “anakupenda kama ulivyo” na tila lila nyingiiiii…..lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna kupinga hilo. Hata kwetu Bongo katika nyakati hizi za utandawazi, wakina kaka wengi wanawaona wanawake kama wakina Naomi Campbell na Jennifer Lopez, ambao wanatamani kuwa nao. Lakini hauhitaji kuwa kama wakina Naomi na Jennifer kumridhisha mwanaume wako, bali hakikisha tu upo katika umbo zuri la kumpelekesha kirahisi kitandani, Basi!
#4 Kuwa Mchokozi. Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi, lahasha! Bali, ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya kingereza unafahamika kama “Tease”, kwa maana hiyo basi tunasema “Tease him”. Cheza nae michezo mbalimbali na burudika nae ipasavyo, na michezo isiwe ya kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po! Kama unataka kuwa mjuzi kitandani, basi unatakiwa umfanye mwanaume wako akutake wakati wote na popote pia. Kujamiiana sio kitasa ambazo unawasha na kuzima mnapokuwa chumbani tu. Mchokoze chokoze wakati mnasakata muziki jukwaani, na mchokoze chokoze (katika mitindo ya kimahaba, bila kuvuka mipaka) wakati yupo na marafiki zake.
#5 Jiamini na Jipende. Ndio, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza maunene, lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba. Hakuna kinacho kera wanaume, kama mwanamke, ambae anauonea aibu mwili wake mwenyewe wakati anafanya mapenzi. Jiamini kuhusu mwili wako wakati upo mtupu, na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kwa-wanawake-tu-fanya-haya-kumchizisha.html