Wednesday, June 3, 2020

JINSI YA KUMSAHAU MPENZI ULIE MPENDA SANA

UTAMUZAIDIAPP

*DARASA

Ni kweli kwamba, mapenzi yanatesa kuliko kitu chochote katika uso wa dunia hii. Ni mapenzi hayohayo ambayo yana nguvu na maumivu makali kuliko maumivu ya kitu chochote unachokijua chenye kusababisha maumivu.

pia ni kweli wapo watu wengi wameumizwa na kuteswa na mapenzi. Wengine wanaendelea kuteseka na kuumia kila siku. Wengine wanatamani kuyaepuka ingawa hawawezi zaidi ya kupumzika kwa muda. Wapo wanaotamani kuyakimbia ila hayakimbiliki. Wengine wanatamani kujiua ila roho wa Mungu anawashindia.
Inawezekana ni kweli mpenzi wako amekuumiza sana lakini vumilia kwani maumivu hayo ni ya muda na ninaamini ipo siku utayasahau.

Maumivu unayoyapata kwa sababu ya mke, mpenzi, mchumba au mume wako ni ya mpito tu, ni kama masika na kiangazi kinavyoikumba aridhi, mara nyingi huwa ni kwa mpito.

Leo nimewaletea tips rahisi ya kuweza kumsahau uliyemuweka moyoni na uliempenda sana na akakuacha bado unampenda

TIPS ZA KUZINGATIA
💎USILIBEBE KAMA VILE NI TATIZO KUBWA SANA. lichukulie kama tatizo la kawaida linaloweza kumpata mtu yeyote na wakati wowote ili uipe akili yako nafasi ya ku relax na kupata maarifa mapya.

💎USIFICHE HISIA ZAKO
Kama umeachwa usione aibu, ongea na ndugu na jamaa zako na uwambie ukweli kuhusu yaliyokutokea, hii itakufanya upunguze mzigo wa nawazo kichwani kwako na kuondoa sumu ya uchungu moyoni na utahisi hali ya wepesi moyoni mwako hasa kwa faraja na ushauri utakaopata. Lakini ukikaa nalo moyoni unaweza ukafa siku si zako kwa presha!

💎FUTA NAMBA YAKE
Kuendelea kua na namba zake kutakufanya uendelee kumpigia ili abadilishe mawazo yake hii itakufanya uumie zaidi hasa kama hakutaki tena na huenda ana mtu mwingine badala yako. Hata kama umezikariri kichwani usiziandike tena kwenye simu yako.

💎USIPENDE KUTEMBELEA AU KUFANYA VITU AMBAVYO MLIKUWA MNAFANYA PAMOJA ENZI HIZO. hiyo inaweza ikakuzidishia maumivu na kumkumbuka.Kaa mbali na vitu vinavyokukumbushia kuhusu mpenzi wako:
Sikiliza nyimbo mpya, weka mbali picha zake na zawadi zote alizokupa, usitembelee sehemu ambazo zinakukumbusha kuhusu yeye. Kua na marafiki wapya ambao hawakumfahamu mpenzi wako.(simaanishi uwaache marafiki wa zamani), pia usijaribu kua rafiki wa mpenzi uliyeachana nae kwani utajikuta unaumia zaidi labda baadae sana ukishasahau.

💎FANYA MAMBO YAKO
Kua bize na mambo mengine;
Fanya mazoezi, katembelee sehemu ambazo hujawahi kwenda na rafiki zako, angalia filamu za mapigano, sikiliza miziki isiyohusiana na mapenzi. Hii itakufanya usahau mapema kuliko kukaa nyumbani peke yako na kuwaza sana kuhusu mpenzi wako

💎USIANZISHE MAHUSIANO MAPYA HARAKA HARAKA. jizuie kuanzisha mahusiano mapya haraka kama vile njia ya kumsahau coz unaweza ukajikuta unapata mtu ambae atakuumiza tena ukazidi kujiona una mkosi.

💎USIMWAMBIE MPENZI WAKO MPYA MABAYA YA MPENZI WAKO WA ZAMANI. Usimwambie mabaya ya mwenzie anaweza akajiona yeye ndio malaika na hivyo akakunyanyasa kwa kukumbushia aliyokuwa anakufanyia mwenzie. Mwelezee mazuri ya mwenzie ili atamani kukutendea mazuri zaidi

💎MSHIRIKISHE MUNGU
Ili uwe huru na uweze kuendelea na maisha yako bila maumivu unatakiwa umshirikishe Mungu kwa imani yako ili aweze kukupa nguvu ya kusonga mbele



source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/jinsi-ya-kumsahau-mpenzi-ulie-mpenda.html

No comments:

Post a Comment