Miaka inavyozidi kwenda mbele uhuru wa binadamu unaongezeka sana kutokana na sera za demokrasia na kudidimia kwa maadili ya kidini, hivyo kuwapa watu nafasi kubwa ya kuingia kwenye mahusiano mapema.
Hali hii pia imechangia kwa ongezeko la kuumizwa kimapenzi kwa watu wengi sana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo tamaa za fedha, usaliti,umbali kati ya wapenzi, shinikizo la wazazi, utofauti wa dini, mitazamo tofauti kati ya wapenzi na kadhalika.
Madhara makubwa sana yamekua yakisababishwa na hali hii ya kuachana ikiwemo watu kujiua hasa vijana, kuathirika kisaikolojia, kufeli mitihani, kuacha kazi na kupoteza muelekeo wa kimaisha kabisa.
Leo naenda kuongelea jinsi ya kumsahau mpenzi wako uliye achana naye na kuanza maisha mapya yenye furaha na amani kama zamani..
Usiyazuie machozi yako:
Maumivu haya yatakufanya ulie sana na kujilaumu kwanini ulipenda lakini ni vizuri kulia sana kadri unavyoweza kwani hii itakupa ahueni na kupunguza maumivu makali unayoyapata.
Futa namba zake:
Kuendelea kua na namba zakekutakufanya uendelee kumpigia ili abadilishe mawazo yake hii itakufanya uumie zaidi hasa kama hakutaki tena na huenda ana mtu mwingine badala yako. Hata kama umezikariri kichwani usiziandike tena kwenye simu yako.
Kua bize na mambo mengine;
Fanya mazoezi, katembelee sehemu ambazo hujawahi kwenda na rafiki zako, angalia filamu za mapigano, sikiliza miziki isiyohusiana na mapenzi. Hii itakufanya usahau mapema kuliko kukaa nyumbani peke yako na kuwaza sana kuhusu mpenzi wako.
Usifiche hisia zako:
Kama umeachwa usione aibu, ongea na ndugu na jamaa zako na uwambie ukweli kuhusu yaliyokutokea, hii itakufanya upunguze mzigo wa nawazo kichwani kwako na utahisi hali ya wepesi moyoni mwako hasa kwa ushauri utakaopata. Pia unaweza kuwaona wataalamu wa ushauri kwa ushauri zaidi.
Usitafute mpenzi mwingine kuziba pengo lake haraka.:
Watu wengi huchukua wapenzi wapya haraka ili kuzuia maumivu lakini hii sio njia sahihi kwani siku maumivu yako yakiisha utagundua kwamba hauna mapenzi ya kweli juu ya huyu mpenzi wako mpya na utaishia kumuumiza tena huyo uliyemchukua.(mwanamke anaweza kujifunza kumpenda mtu lakini mwanaume asipokupenda mwanzoni hawezi kujifunza kukupenda hata iweje)
Andika mapungufu yake kwenye karatasi:
Jaribu kukumbuka matatizo na mapungufu ya huyo mpenzi wako hii itakufanya uone kwamba hakuna madhara uliyoyapata ila faida na itakupunguzia machungu yako.
Msamehe mpenzi wako ata kama hajakuomba msamaha:
Njia pekee ya kua huru kihisia ni kusamehe, visasi moyoni havitakusaidia kabisa kuondokana na maumivu na utajikuta unawaza kufanya mambo ya ajabu ambayo yanaweza kukuletea matatizo ikiwemo kumuua au kumjeruhi.
Kaa mbali na vitu vinavyokukumbushia kuhusu mpenzi wako :
Sikiliza nyimbo mpya, weka mbali picha zake na zawadi zote alizokupa, usitembelee sehemu ambazo zinakukumbusha kuhusu yeye. Kua na marafiki wapya ambao hawakumfahamu mpenzi wako.(simaanishi uwaache marafiki wa zamani), pia usijaribu kua rafiki wa mpenzi uliyeachana nae kwani utajikuta unaumia zaidi labda baadae sana ukishasahau.
Usiseme mabaya kuhusu mpenzi wako au familia yake:
Hii ni hali ya mpito tu, ukianza kupost vitu vya ajabu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano yako haitakusaidia kitu bali kujiabisha kwa jamii na siku maumivu yakiisha utajuta sana kwanini uliandika mambo hayo. Hili ni tatizo sugu kwa watu wengi walioachana kupost vitu kama kumkomesha mpenzi wake wa zamani. Naomba nikwambie mapenzi hayana kisasi kama umeachwa, umeachwa tu. kumbuka silence is the best weapon..
Fikiria faida za kuishi bila mpenzi:
Kua peke yako kuna faida nyingi ikiwemo kua huru na maamuzi yako, kuchagua marafiki unaotaka, kujikinga na magonjwa ya zinaa,kuishi maisha unayotaka bila kuhofia kukosolewa, unaweza kuzima simu yako ata wiki nzima bila hofu, kulala peke yako bila bugudha, kupunguza msongo wa mawazo ambao hutokana na ugomvi wa mara kwa mara.
tumia dawa za kupunguza mawazo ; wakati mwingine maumivu ya kuachana na mpenzi yanaweza kua makali sana, mtu akshindwa kupata usingizi, kufanya kazi zake, kukosa furaha kabisa na kulia kila siku. hii huathiri sana mfumo wa maisha husika na huweza kusababisha mtu kuamua kujiua kabisa kama mnavyosikia watu waliojiua sababu ya mapenzi. ndio maana kuna dawa maalumu za watu wenye msongo wa mawazo. ukitumia dawa hii mwili unatulia na ubongo unapumzika sana. itakupa usingizi na kila ukiamka unakua na furaha upya na unaendelea na maisha yako kama kawaida. dawa hizi zinaharakisha sana kusahau na kuendelea na maisha yako haraka kuliko kujaribu kupambana mwenyewe.mfano wa dawa hizo ni bupropion,clomipramine na doxepin. zinapatikana maduka makubwa ya madawa kwa gharama kubwa kidogo lakini ni bora kuliko kuendelea kupoteza muda kumuwaza mtu ambaye hakutaki tena kwani hiyo ni gharama kubwa zaidi.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/saikolojia-hizi-ndio-njia-kumi-na-moja.html
No comments:
Post a Comment