Monday, June 15, 2020

Si kazi ya mchepuko wa Mwanaume wako kuiheshimu ndoa yenu, bali ni kazi ya mume wako kuiheshimu ndoa yenu.


Kumbuka, wewe na mume wako pekee nd'o mlisimama mbele ya madhabahu na kula kiapo cha ndoa, hivyo acha kupigana na mtu wa nje ambaye hakuwepo wakati mnakula kiapo.
Hivi, utapigana na wanawake wangapi kabla hujagundua kuwa Mume wako ndio haheshimu Kiapo mlichoapa?.
Haijazoeleka, lakini Muda mwingine ukweli ni vizuri usemwe, dili na Mume wako.
Kabla hujaanza kuusifia mchepuko wako kuwa unajua kujali kuliko mume wako kwakua tu unakununulia vichupichipi, vimauamaua, kukutoa out kwa chakula mara kwa mara, mshukuru kwanza mume wako kwa kukupa chakula mpaka ukapata nguvu ya kuchepuka, kulipa ada za watoto, kuhudumia ndugu zako, kukupa nyumba ya kuishi na majukumu mengine ambayo ukiachika mchepuko utayakimbia.
Share
Image may contain: 1 person, sitting


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/si-kazi-ya-mchepuko-wa-mwanaume-wako.html

No comments:

Post a Comment