Wednesday, June 10, 2020

KWANINI MWANAMKE NDIYE SABABU YA MAFANIKIO YA MWANAUME πŸ€”

UTAMUZAIDIAPP
Sio rahisi kwa Wanaume wepesi wale wanao mchukulia Mwanamke kama CHOMBO DHAIFU huku kutwa wakiulizana:-
πŸ‘‰πŸΌ NANI KAMA MAMAπŸ˜‚πŸ˜‚
Kwa akili ya kawaida hapa namzungumzia MWANAMKE huyo huyo ambaye ni Sawa na Mama wa kukuzaa, Huyo ndiye sawa na Dada yako, Huyo huyo ni sawa na SHANGAZI YAKOπŸ’―
Haina maana kwa Mwanaume kuamini Mwanamke mwenye HESHIMA NI MAMA au wale wanaotokana na jamii yake
Mwanamke ni jinsia, usipomheshimu wewe Mtoto wa kiuno chako atamheshimu na kumpa THAMANI zaidi yako.
Maisha Mazuri ya Mwanaume yanatokana na juhudi zake huku akiwa na Mwanamke wa mipango, Kwani wanaume sahihi wanaweza kutafuta pesa lakini namna nzuri ya kuzitumia pesa hizo ni mpaka awe na MKE MWEMA πŸ’ͺ🏼
Siwaongelei wale wanaume wanaosubiri chakula mezani huku hawajui kimetoka wapiπŸ˜‚
Mwanaume ninae msemea hapa ni yule:
πŸ‘‰πŸΌAJUAYE MWANAMKE ANAHITAJI KUTUNZWAπŸ’―
Usiwe mjinga kuamini Mwanamke sahihi kwako ni NDUGU YAKO kwani hata yeye thamani yake inaweza kutajwa na wewe peke yako ila Wanaume wenzio wakamchukulia kama unavyomchukulia Mwanamke wako, Mheshimu Mwanamke kwani kwa maisha ya Mwanaume haijalishi ni nduguyo ila neno moja uliweke akilini MWANAMKE NI MTU MUHIMU MAISHANI MWAKO kama hutajua leo iko siku utajua.
ANGALIZO;-
πŸ‘‰πŸΌSIO KILA MWANAMKE ANAFAA KUWA MKE WAKO
Mwanamke mmoja ndiye atafaa kuwa MKE wako haijalishi wajihi wake, Muonekano wake lililo la thamani kwako AKUELEWEπŸ’―
Huyo ndiye atakufikisha kwenye MAFANIKIO YAKOπŸ’ͺ🏼


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/kwanini-mwanamke-ndiye-sababu-ya.html

No comments:

Post a Comment