Monday, June 15, 2020

#_HIVI UNAWAJUA WATU #_HATARI KATIKA #_MAISHA YAKO..??


๐ŸŒพMoja ya watu hatari katika maisha yako ni wale ambao wanaangukia kwenye kundi la “Silent Enemies”(Maadui wa kimyakimya wanaojificha). Mara nyingi watu hawa hufanya kila mbinu za kuwa karibu na wewe ili wakufahamu kwa undani na iwe rahisi kutumia taarifa zako kutimiza haja zao.
Kuna watu wengi sana wameumizwa na kundi hili kwani hawakutarajia watu hawa wangefanya walichofanya.
.
Kuwagundua watu hawa sio kitu kirahisi sana ila katika maisha yangu imeshawahi kutokeza zaidi ya mara moja kujikuta katika matatizo makubwa yaliyosababishwa na watu wa namna hii.
Kuna mambo muhimu nimejifunza ya kutusaidia siku zote:
.
1)๐ŸŒพNi muhimu sana kujua “Intentions” za watu ambao wanakuja karibu yetu.Mara nyingi moyo wa mwanadamu ni kiza kinene sana ila ukiwa makini zaidi unaweza kuvumbua mapema.
Kuna wale ambao unakuta wanataka sana kujua details zako binafsi kwa haraka sana hata kama hamjazoeana sana,kuna wengine wanajitahidi kujionyesha ni wa muhimu sana ili uwaamini mapema na ujifunue kwa haraka:
Ukiona mtu anataka sana kukujua katika mambo binafsi na bado hamjawa karibu sana,ni vyema ukawa makini zaidi.
.
2)๐ŸŒพJifunze kuamini watu taratibu.Kumbuka kumpenda mtu haina shida ila kumuamini ni mchakato.(Love is a feeling but trust is earned). Usiwe mtu ambaye mtu kidogo tu umeshamuamini.Kuna watu ambao wanakumbuka walitapeliwa,waliingizwa kwenye mitego ama walichafuliwa jina kwa sababu kuna mtu walimwamini kuliko kawaida.
Waamini watu kwa awamu awamu.Kuna watu wakishakuwa karibu na wewe chochote watakachosema kuhusu wewe katika jamii wataaminiwa hata kama wanadanganya.
.
3)๐ŸŒพUsidharau “Intuition” yako.Kila wakati kuna sauti ndani itakuwa inakuonya kuhusiana na mtu fulani.Mara nyingi inapokuambia kunaweza kusiwe na dalili yoyote ile ya kuonyesha kuwa huyo mtu ana matatizo ama anaweza kusababisha matatizo.
Watu wengi kwa sababu hii hupuuzia na kudharau “taa nyekundu” inayowaka ndani yao kuhusiana na mtu fulani,mwisho wa siku wamelia.
๐ŸŽบUkisikia sauti hii,usipuuze ukaja kujuta baadaye,Chukua hatua ya haraka kumwepuka mtu huyo.
KAMA UMEJIFUNZA KITU,SHARE KWA GROUPS 5,
Zeuzedric Benson
Image may contain: 2 people, people standing


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/hivi-unawajua-watu-hatari-katika-maisha.html

No comments:

Post a Comment