Wednesday, June 10, 2020

WANAUME WALIOOA/WANAOISHI NA WANAWAKE/ANAKUAMBIA ANA MTU WAKE

utamuzaidiapp
Unakutana na mwanaume, anakuambia nimeoa lakini nakupenda, kwa waisalamu dini inaruhusu kuoa wake wawili lakini usiingie kichwa kichwa, kuna tofauti ya mtu kutaka kuoa wake wawili na kuchepuka. Mara nyingi hana mpango wa mke wapili bali kukufanya mchepuko, lakini achana na hao, unakutana na mwanaume anakuambia kabisa nimeoa, nina mtu wangu tunaisni naye na tuna mtoto au anakuambia kuwa kuna mwanamke nipo naye hatusihi pamoja.
Anaendelea kukuambia kuwa sasa hatuko vizuri nakaribia kumuacha. Dada yangu hakuna kitu kinaiotwa “Nakaribia kumuacha!” mwanaume akimchoka mwanamke anamuacha hakaribii wala hapigi hodi kumuacha. Kwa maana hiyo mwanaume akikuambia nina mtu wangu, awe mke, mpenzi au nani anakaribia kumuacha basi jua kuwa unadanganywa. Lengo lake ni kuchepuka kwa uhuru, usimsumbue anapoacha kupokea simu zako wala usitake aende kwako.
Lakini kuna wale wanakuambia kuwa kuna mwanamke mwingine nipo naye, sijajua kuwa niwe na yupi. Anakuambia kuwa anakupenda lakini ana mpenzi mwingine hivyo anakua nawewe atachagua baadaye, dada yangu hapo ushaliwa. Ukiona kakuambia hivyo jua anampenda sana huyo mwanamke wake, anakuambia ili siku akiwa na mwanamke wake usipige simu, akikuambia kuwa anaenda kwa mwanamke wake usimsumbue.
Unapoamua kubaki na mwanaume wa namna hii basi jua kuwa kila kitu ni bahati na sibu, kwamba anaweza kumucha mpenzi wake lakini pia anaweza simuache, ukitaka kujua kuwa wewe ndiyo anakudanganya hembu jaribu kumuambia ampigie simu na huyo mwanamke mwingine amuambie kuwa ana mwanamke mwingine ambaye ndiyo wewe uone kama tafanya hivyo? Kua makini na ikiwezekana kimbia kabisa mwanaume anapokuambia kaoa, anaishi na mtu au ana mtu wake, hamuachi angekua wa kumuacha angeshamuacha kitambo!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/wanaume-waliooawanaoishi-na.html

No comments:

Post a Comment