Thursday, June 11, 2020

WEWE NI MZURI TU HATA KAMA WANAKUSIMANGA SONGA MBELE UTAPOKEA BARAKA NA KUJAA TELE.


.
Sio kila mtu Kwenye huu ulimwengu atakupenda na haijalishi Ni nini unafanya kwa ajili Yao.
Unaweza kuwa mrembo na mtanashati lakini sio kwamba kila mtu atavutiwa na Utanashati au urembo wako.
Unaweza kuwa mtenda mema kwa watu na mwenye kujitoa sana kwa watu lakini Haina maana kwamba kila mtu atakupenda.
Malipo yako kwa Mungu na unaweza kuwa huoni faida lakini kipato unachopata kinatokana na baraka zake anazokupa kwa kubadili ubaya wao kuwa wema.
Watu wengine watakuwa wakali kwako na kukukemea au kukusemesha kwa ukali sana bika hata sababu. Na baadhi yao Wanaweza kukuchukia sana As if umewatendea ubaya wowote lakini hapana.
Lakini usiwaache watu wachache wanaokuchukia, wanaokukejeli na kukubeza wakakufanya ukabadili nafsi yako iliyo njema ambayo Mungu alikuumba nayo.
Nakushauri usiingie kwenye mtego huo ni wa shetani.
Usiwaruhusu wakakufanya ukawa na roho mbaya isiyotamanika kwa watu na jamii kwa ujumla. Wasikufanye ukawa mtu mbaya asiye mwema na mtenda mabaya.
Wema wako na matendo mema Unayo yafanya yanakufanya Uwe mtu mwema Kuliko unavyo fikiria.
Usiige maisha ya watu wala usibadilishe Utu wako mwema kwa sababu Kuna watu fulani hawapendezwi na namna unavyoishi.
WEWE NI MZURI, WEWE NI MWEMA. USIJARIBU KUWA MTU MWINGINE KUWA WEWE.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/wewe-ni-mzuri-tu-hata-kama.html

No comments:

Post a Comment