Monday, June 15, 2020

Kama unataka KUSTAWI na KUFANIKIWA." USIOLEWE ILI UKATUNZWE:

"We dada bado hujaolewa halafu una Boyfriend, MUNGU Hawezi kukuletea ZAWADI yako (Mume Wako Mzuri, ZAWADI Nzuri) wakati tayari USHAJIWEKEA Himaya yako, tayari Ushajiwekea UZIO, tayari una Boyfriend ……., Unataka Mume Mzuri? Unataka ZAWADI Nzuri toka kwa BWANA? AMUA Kuishi Maisha MATAKATIFU, ZAWADI yako ITAKUJA."
TAFAKARI:
-"Mvulana amekuita, amekuambia Njoo Chumbani kwangu, UMEINGIA ndani Chumbani KWAKE.......Ameanza Kukushikashika (Anakutomasa), Wewe unaanza kusema "SHINDWA shetani, SHINDWA shetani....." Kamwe shetani HATASHINDWA hapo, maana NENO Linasema IKIMBIE ZINAA na SIO WEWE KUENDELEA KUKAA Hapo na Kuanza Kusema USHINDWE shetani,......... HAKUNA.
ISHI MAISHA MATAKATIFU Kama unataka KUSTAWI na KUFANIKIWA."
USIOLEWE ILI UKATUNZWE:
Usijione kwa sababu Wewe ni Mtoto wa Kike ndio unastahili kuwa pangu pa Kavu, ACHA UJINGA. Usifanye KUOLEWA ndio SULUHISHO la Matatizo yako, ndio SULUHISHO la UCHUMI wako.
Kuna mabinti sijui ni Uchovu au kukata tamaa, utawakuta wanalia na kuomba “Bwana YESU nipe mume nataka kuolewa, anachana Nywele kwa Mtindo mbalimbali ili Vijana wamuone, huo ni UJINGA.
USIOLEWE ili UKATUNZWE, OLEWA ili Kutimiza MAKUSUDI YA MUNGU, HUOLEWI ili Mtu AKUTUNZE, Unaolewa kwa sababu unataka kutimiza RATIBA YA MUNGU, Sio Unaolewa kwa sababu unaona pale Nyumbani WAMEKUCHOKA au maisha ni magumu, HAPANA.
OLEWA kwa sababu UNATIMIZA Makusudi na Ratiba ya MUNGU kwani Yeye amesema si vema mtu awe peke yake.
I do ❤️efatha


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/kama-unataka-kustawi-na-kufanikiwa.html

No comments:

Post a Comment