Thursday, June 11, 2020

KUPUUZANA KUNA DHOOFISHA MAPENZI KULIKO KUMPUUZA MWENZA WAKO BASI ZUNGUMZA NAE KINACHOKUTATIZA NA KWA KUFANYA HIVYO UTAKOMBOA UHUSIANO WENU.

UTAMUZAIDIAPP
Mahusiano mengi yameghubikwa na UBINAFSI pamoja na WATU kujihesabia haki hata kuleta sintofahamu upande wa pili, Kwa sasa ili mtu ajione ni MBABE basi yupo tayari kuonyesha dharau kwa mwenza wake kitu ambacho ni hatari sana, Kama kuna tatizo KAENI MUONGEE mjue namna ya kumaliza tofauti yenu, Kama mmeshindwa kukaa wenyewe shirikisheni hata wazazi, Kama imeshindikana kote huko BASI VUNJENI UMOJA WENU kuliko kuishi nyumba moja na hamuongei kumbe kilichowatoa majumbani mwenu kuja kuunganisha MIILI YENU NI NINI?
Unajua wengi hawajui kwamba KURUHUSU UFA KWENYE MAPENZI ni kuruhusu Mtu mwingine kuingilia penzi lako, Imagine Mtu yupo na stress zako halafu anatokea mtu anamponya kwa kumpa POLE unadhani utabakia salama?
Mapenzi sio vita, bali Mapenzi ni uwanja wa MAHABA kwamba muda wote ni vionja vya mwitikio wa HISIA lakini kama mnatengeneza UFA ninyi wenyewe Basi msitafute MCHAWI ikifika TAMATI.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/kupuuzana-kuna-dhoofisha-mapenzi-kuliko.html

No comments:

Post a Comment