Friday, June 12, 2020

KAMA UNAISHI NA MWANAUME AMBAYE HUJUI KWAKO, HUMJUI NDUGU YAKE YAKE YOYOTE, FANYA HIVI.

UTAMUZAIDIAPP

Kama unaishi na mwanaume ambaye hujui kwao, huajwahi kufika kwao, humjui ndugu yake yoyote zaidi ya wale ambao anakuambia kuwa ni ndugu zake unaongea nao kwenye simu! Kisa tu kakuambia muishi pamoja kwanza lakini hajawahi kukupeleka hata kwao na hapa simaanishi yeye kuja kwenu kujitambulisha hapana wewe hujawahi kwenda kabisa kwao, hapa simaanishi kijijini, wakati mwingine kijijini inaweza kuwa mbali lakini hata kwa ndugu yake yoyote ambaye ni wa hapo mjini!
Ila kama hana ndugu mjini basi huko kijijini hajakupeleka hata siku moja angalau wakakujua, lakini wewe ukajitia kiherehere hata bila ndoa ukajibebesha na mimba na kuanza kuishi naye basi jua kuwa wewe ni tatizo kuliko huyo mwanaume! Mwanaume umekutana naye kimjini mjini hata Shangazi yake wa uongo humjui ushanyanyua kila kitu na kujipeleka kwake basi jua kuwa wewe hujielewi! Tena mwingine unaishi au umejuana na mwanaume mwaka mmoja hajawahi kugusia hata ndugu zake, hajawhai kukuonyesha mtu yeyote anayehusiana naye kidau zaidi ya wale rafiki zake walevi wenzake!
Lakini mwingine umejuana naye miezi miwili ushaanza kujiona mke wake kabisa, unajipangia na kutaka hata kuzaa sijui nini na nini? Dada yangu hujielewi kabisa, hembu kama umeona basi huwezi kusubiri hiyo ndoa ndiyo ubebe mimba basi angalau jua kwao ujue kuwa hajaoa! Acheni huu ujinga wa mwanaume aliniambia hivi mwanaume aliniambia vile, mshajua wanaume wengi ni waongo, mwanaume atakuambia kile unachotaka kusikia tu ili kukufurahisha hivyo unapofanya maamuzi ya kuishi na mwanaume acha kufanya maamuzi kwa kusema kaniambia hivi na vile bali fanya maamuzi kwa kumchunguza na kujua ukweli wako!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/kama-unaishi-na-mwanaume-ambaye-hujui.html

No comments:

Post a Comment