Thursday, June 11, 2020

NI KAZI YAKO BABA KUMLINDA MWANAO HATA KAMA NI DHIDI YA MAMA YAKE!

UTAMUZAIDIAPP
Nilazima umfundishe mwanao wakike kua ana thamani kuliko muonekano wake wa nnje, hii ni kazi ya Baba zaidi kuliko Mama, nasema hivyo kwakua baadhi ya wanawake kutokujiamini kwao kuhusu muonekano wao hupelekea mpaka kwa watoto wao mpaka kufikia kuwafanya watoto waamini kua ili uwe mzuri nilazima uwe mweupe, uwe na nywele ndefu na uwe na tako kubwa.
Kuna wanawake wengi wananyanyasika na kuhangaika juu ya namna wanavyoonekana, lakini mahangaiko yao hayaishii kwao tu, huendelea mpaka kwa watoto. Wanawahangaisha katika kuwasuka watoto wadogo mitindo ya watu wazima, kuwapaka madawa na mambo mengine ya ajabu ajabu. Kwa Mama anaweza kuona haina madhara nampendezesha.
Lakini kwa mtoto wa miaka sita saba ni kama unamuambia wewe si mzuri vyakutosha hivyo unatakiwa kuongezea hiki na kile. Hapa simaanishi kwamba usimsuke mtoto wako na wala usimpendezeshe, hapana lakini hembu acha kumpaka vitu ambavyo vitabadilisha kabisa muonekano wake, hasa ngozi yake, lakini pia kama ni nwele mtengeneze mitindo ya watoto ambayo haimfanyi kuwa tofauti na watoto wa umri wao.
Narudia mwanamke ambaye anaamini katika mkorogo na tako kubwa ni ngumu kunielewa lakini mwanaume ni kazi yako, hembu waka kipimo kuwa utamfanyia hiki mwanangu lakini hiki hapana. Kama unataka picha za Instagram jipige mwenyewe lakini si mwanangu (hawaweki picha halisi wanataka mtoto awe mzungu kwanza!), gombana kwaajili hilo lakini mlinde mwanao kwani usipofanya hivyo Mama yake atamharibu akidhani anamtengeneza kumbe anamuathiri kisaikolojia.
Iko hivi nirahisi mwanamke anayejihisi mbaya kunyanyasika kuliko yule ambaye anajihisi mzuri. Muambie mwanao kua ni mzuri na unampenda, mpe thamani yake na mfanye atambue kuwa ana thamani kuliko aina yoyote ile ya manukato au urefu wowote ule wa nywele. Mtoto ambaye hajiamini nirahisi kunyanyaswa kijinsia kwani anakua haamini kama ni mzuri na atafanya kitu chochote ili afiti katika mazingira yoyote.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/ni-kazi-yako-baba-kumlinda-mwanao-hata.html

No comments:

Post a Comment