Ubaya wa wanawake ni wagumu kuelewa, wakishapenda wanadhani kuwa mapenzi yanatosha, ipo hivi mapenzi yanatosha kama wote mnapendana. Ukikutana na mwanaume akakuambia kuwa “Nina mtu lakini nataka kumuacha polepole ili nisimuumize!” Basi jua kuwa huyo mtu hakupendi na anachotaka ni kuchepuka kwa uhuru, kwanza wewe ndiyo mchepuko ndiyo maana huyo mwingine hataki kumuumiza, hakuna cha kuacha taratibu na hakuna namna ambayo unaweza kumuacha mtu bila kumuumiza kama kweli alikua anakupenda!
Kwanza kuacha polepole ndiyo nini kwamba unamkaanga au unamuacha kwa kumuwekea kachumbari! Ni sawa na kusema eti namchinza polepole tena ndiyo yenye maumivu makali zaidi, hembu fikiia unamchinja kuku polepole, unajua kuwa atakufa lakini unamchinja polepole. Kwanza niseme kuwa wewe unayeambiwa na ukakubali kuwa mwenzako aache polepole na huyo anayekuambia kuwa anaacha polepole wote ni washenzi tu, narudia wote ni washenzi tu! Hembu fikiria upo na mwanaume.
Unajua anakupenda kumbe anakuacha polepole, kwamba kila sikua anakuja kwako, kila siku anakutumia meseji, anakuambia hana mtu anakudanganya atakuoa unabeba na mimba yake kumbe mwenzako ana mtu wake na washakubaliana kuwa wakuache polepole. Anakupotezea muda, unakaa miaka miwili na mwanaume anayekuacha polepole, unakataa wachumba, unakataa madanga kisa una mtu wako anayekuambia kuwa anakuacha polepole, si ushenzi huo. Nashindwa hata kuwalewa nyie wanawake mnaoambiwa hivyo.
Uko na mwanaume anakuambia nina mtu naishi naye nitamuacha polepole, nina mke, mpenzi, nimezaa naye, kwamba hiyo polepole wanakua wanafanya mapenzi nusunusu au? Mwanaume akikuambia hivyo basi jua kuwa huyo mwanaume ni MSHENZI na kakudharau, lakini wewe ukikubali hivyo basi jitafutie tusi mwenyewe kwani unadanganywa! Hakuna kitu kama hicho, ukiona unaambiwa hivyo jua huyo mwanaume hakupendi wewe ni mchepuko narudia wewe ni mchepuko na kama ni mume wako basi jua kashafikia kiwangi kikubwa cha umalaya wala hajali kama wewe ni mkewe au binamu yake! #share
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/kama-unasubiri-amuache-taratibu.html
No comments:
Post a Comment