Makala hii ni katika kujibu maswali mengi na mapovu ya wasomaji wangu kuhusiana na Makala yangu ya nyuma nikielezea kuwa, si lazima mwanaume kumshirikisha mwanamke katika mambo yake na kisheria Mali alizochuma mwana ndoa kama zina majina yake ni zake hivyo mwenza wake hawezi kuzidai. Nitajibu maswali haya moja kwa moja kwa kuangalia Comment za wasomaji wangu.
MSOMAJI 1; Ama kweli wahenga walisema hakuna mkamilifu duniani ALLAH pekee,Yani we leo wa kuandika utumbo namna hiyo! Wakati anajenga sawa mimi sijachangia hata mfuko lkn je alikuwa anapikiwa kwa mm nitilie nguo anafuliwa kwa dobi! Hivyo vyote haivitoshi je khs burudan 6/6 maombi ili afanikiwe? Na hivyo vichache ndo vilivyompa utashi was kuvipata iweje avinihusuuuuu......?
JIBU; Ni kweli, kifungu cha 114 cha sharia ya ndoa namba 29 kinaipa mahakama kusimamia mgawanyo wa mali pale wahusika wanapoachana. Hakuna kugawana nusu kwa nusu bali mahakama itaangalia mchango wa mhusika. Kama wewe ni Mama wa nyumbani basi itakupa kulingana na mchango wako.
Changamoto ya hiki kipengele ni hivi, Mgawanhyo unakuja wakati wa kuachana lakini si wakati wa ndoa. Kwa mfano, mmenunua gari lina jina la mwanaume basi anaweza kuliuza bila kumshirikisha mke, mmejenga nyumba, ina jina la mwanamke anaweza kuiuza au kuichukulia mkopo bila kumshirikisha mke. Kwa maana kuwa mwana ndoa huwezi kumzuia mwanza wako kutumia mali ambazo zina majina yake kwa namna anavyotaka yeye.
VIPI KUHUSU NYUMBA MNAYOISHI; Hii kimombo inaitwa MATRIMONIAL HOME, nyumba mnayoishi bila kujali mmiliki ni nani kifungu cha 59 cha sharia ya ndoa inakataza mmoja wenu kuiuza, kuchukulia mkopo, kupangisha au kuifanyioa chochote kila bila ridhaa ya mwingine. Kwa maana kuwa, nyumba pekee ambayo hawezi kuuza ni hii ambayo mnaishi, nyingine kama zina majina yake ni zake anaweza kuzifanyia chochote.
MSOMAJI 2; Hakunaga hati yenye majina ya watu wawili, Mali iliyopatikana wakati wa ndoa iwe ya mme au ya mke niya wanandoa wote, haijalishi mmoja ana kazi ama la,as longer as imepatikana wakati wa ndoa na ndoa inatambulika kisheria. Rejea vizuri sheria ya ndoa.
JIBU LANGU; Kwanza kuna hati yenye majina hata matatu, hivyo mali inaweza kuandikwa majina mawili, matatu na hata manne. Pili si kila mali iliyopatikana wakati wa ndoa ni ya wote, hapana kila mwana ndoa anaruhusiwa kumiliki mali yake binafsi. Labda nikurudishe kwenye sharia ya ndoa namba 29 kifungu cha 58 ambayo inasema.
58. Subject to the provisions of section 59 and to any agreement to the contrary that the parties may make, a marriage shall not operate to change the ownership of any property to which either the husband or the wife may be entitled or to prevent either the husband or the wife from acquiring, holding and disposing of any property.
Kwa Tafsiri isiyorasmi wanasheria mtanisaidia kwa wale ambao hawalewi Kipare kifungu hiki kinasema “Kwa kuzingatia kifungu cha 59 (Kifungu cha 59 kinazungumzia nyumba wanayoishi wanandoa ambayo huwezi kuigusa) na makubaliano mengina ambayo yaliingiwa na wote, ndoa haiwezi kubadili umiliki wa mali au kumzuia mume au mke kutafuta, kumiliki na kuitumia mali ya aina yoyote.”
Sijui hata kama mmenielewa maana na mimi kipare changu ni cha shida shida, ila ni hivi, mume au mke anawez akumiliki mali, kuifanyia chochote kile mali yenye jina lake na mwingine hana haki ya kumzuia. Mali pekee ambayo ni lazima kumshirikisha mwenza wake ni ile yenye majina yao wote, nyumba ambayo wanaishi au mali ambayo walikubaliana iwe yakwao.
USHAURI WANGU; Kulikua na mapovu mengi kuhusu hii mada, lakini shida nikuwa sharia sijaandika mimi. Ila unachotakiwa hasa wanawake, wanaume sisi tunajiongeza ongeza, hakikisha na wewe unakau na chakwako, nyumba mnayoishi ni yakwenu hawezi kukufukuza ila nyingine kishertia kama zina majina yake ni zake hata kama ulichangia.
Lakini pia, suala la kugawana mali linakuja wakati wa kuachana, kama bado mpo kwenye ndoa hakuna kuachana basi hakuna kugawana. Fanya kazi, kama unafanya kazi absi nyumba ya kwanza kaandika jina lake ya pili jina lake hapana, kama na wewe umechangia basi komaa na wewe uandikwe maana hujui kesho ikoje. Kama huchangii basi tafuta ili na wewe uwe na kakitu kidogo.
NB; Mimi sio Mwanasheria hivyo wale Wanasheria Wasomi mnakaribishwa kufafanua zaidi.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/je-mali-zinzopatikana-wakati-wa-ndoa-ni.html
No comments:
Post a Comment