Najua kweli una matatizo unaumia labda umpweke sana, lakini unajua namna unavyozidi kulalamika na kujionea huruma ndiyo unavyozidisha maumivu? Kuna watu wengi wana matatizo makubwa kuliko wewe, lakini hawana namna, wanalazimika kutoka na kufurahia maisha yao.
Unalia na kulalamika kila siku, kuwa wewe hujaolewa, labda unajiona mbaya kisa huna tako kubwa au sijui labda wewe ni mwembamba sana huna mguu wa bia. Unalia, hivi unajua kuwa kuna ambaye hana tako kabisa, ndiyo, wewe si una la kukalia, kuna mamia hawana hata hilo la kukalia.
Unalia huna mguu wa bia lakini unaweza kutembea, hivi unajua kuwa kuna ambao hawana miguu kabisa, lakini huwaoni wakilialia, wamekubaliana na hali hiyo ya maisha. Umekaa na mwanaume anakunyanyasa kila siku hutaki kuondoka halafu unalia kana kwamba anajali kuwa una machozi.
Eti kisa umezaa tu, una mtoto kabla ya ndoa unajionea huruma, unajiona kama unamatatizo sijui una mikosi huwezi kuolewa tena. Ndugu yangu hivi unajua kuwa kuna mamilioni wanatafuta hicho kizazi bila kujali wanalia nyumbani au chooni lakini hawakipati!?
Ndiyo hujabahatika kupata mtoto, unalia kila siku, unaruhusu watu wakunyanyase, unaruhusu vipigo na mateso kisa mtoto, hivi unajua kuna ambao sio kama tu hawana watoto, lakini wanaumwa mahututi kitandani na hawawezi hata kufanya chochote!?
Kuna mambo mengi ya kumshukuru Mungu kuliko yale ya kulalamika. Kama unataka kuwa na furaha ya kweli nilazima uanze kwa kufurahia vitu vidogovidogo ambavyo Mungu kakubariki navyo. Hembu kama unakitu cha kumshukuru Mungu comment "Ahsante Mungu"
Ili kujifunza zaidi namna ya kutunza na kuimarisha Ndoa, Uchumba/Mahusiano yako na kupata ushauri wa kisaikolojia, ungana nasi katika group letu la whatsApp "ITUNZE NDOA YAKO" kwa kunitumia ujumbe wako kwenye whatsApp inbox yangu kwa nambari 0717 442 212.
Au bonyeza link hapo chini ikupeleke moja kwa moja kwenye whatsApp inbox yangu
πππ
πππ
Share
Like Page
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/najua-kweli-una-matatizo-unaumia-labda.html
No comments:
Post a Comment