Tuesday, June 2, 2020

SIO LAANA, KAMA NI SINGLE MOTHER ACHA KUMFICHAFICHA!

UTAMUZAIDIAPP
Kama wewe ni Single Mother, unapotongozwa, ku cha kwanza kabisa wakati unajitambulisha, mmetoka out hata kabla hamjafanya chcohote na mwanaume hakikisha kuwa unamuambia kuwa una mtoto. Kama unajisikia vibaya kusema kuwa wewe una mtoto kwanini unataka mwanaume kujisikia vizuri kuoa mwanamke mwenye mtoto?
Iko hivi, kwenye vitu ambavyo huwezi kuficha ni mtoto, hata kama yuko kwa Baba yake, hata kama analelewa na Mama yako, lakini kama ulishawahi kuzaa basi una mtoto na una wajibu wa kumuambia mwanaume wako kuwa una mtoto ili aamue yeye kuwa anaweza kuoa mwanamke mwenye mtoto au la.
Mtoto si laana, na wala mtoto hazuii mwanamke kuolewa, ndiyo maana kuna wanawake kibao wana watoto wao wameolewa na kuna wanawake kibao hata hawajawahi kuguswa lakini hawajaolewa. Mtoto anakua tatizo pale wewe mwanamke unapomuona mtoto wako ni tatizo. Tuseme tu ukweli, kama wewe mwanamke, Mama, umebeba mimba miezi 9, ukakaa Leba, ukasukuma, au ukapasuliwa ukauguza kidonda.
Ni mtoto wako, lakini unaona aibu kusema kuwa mimi nina mtoto mmoja anaitwa Caren, ukatoa na kapicha ka mwanao kwenye Pochi yako ukamuonyesha, yaani wakati unamtaja mwanao ukamtaja kwa raha zote kama unafika kileleni, unamficha ficha, wewe Mama yake unaona aibu kusema nina mtoto, halafu unataka mwanaume ambaye kakuona jana, ambaye hana uchungu na mwanao yeye ampende mwanao?
Eti unataka mwanaume amkubali kumlea wakati wewe mwenyewe hutaki hata kukubali kuwa umezaa? Dada zangu mtoto sio laana, ila kama wewe mwenyewe unamficha ficha, ukiitwa Mama unanuna, yaani hata rafiki zako hawajui kama una mtoto basi juwa kuwa hakuna mwanaume ambaye atampenda.
Kwa bahati mbaya ni kuwa, mtoto hafichiki, na kwa bahati mbaya zaidi nikuwa wanaume si kama wanawake. Mwanamke unaweza kuwa na watoto kumi, ukamficha, akajua akakusamehe na ndoa mkafunga, au akajua mkiwa kwenye ndoa akakusamehe na kusaidia kulea ila mwanaume ukimdanganya hata kama mmeingia kwneye ndoa anaweza kugeuka na kukutelekeza.
Nimechoka kuandika, aisee, mtoto si laanaa! Mtoto si laaana! Si laana, ni Baraka! Baraka! Baraka! Acha kumficha ni wako, any way


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/sio-laana-kama-ni-single-mother-acha.html

No comments:

Post a Comment