Mwaka jana mwezi, nakumbuka ilikua ni tarehe kumi na mbili, ndiyo siku nilinunua Kitabu chako na kwakua nilikua na shida sana nilikisoma chote siku moja. Baada ya kumaliza kukisoma nilikupigia simu na kukuambia hakijanisaidia, nilikuambia yote uliyoyaandika hapa nimeyasoma lakini ulinibishia na kuniambia hapana.
Kama ungeyafanya haya basi ungekua na furaha na usingeongea hivyo, nielezee shida zako. Nilianda kukuambia kuhusu tabia ya ulevi ya mume wangu, nikakuambia namna ambavyo anabadilisha wanawake kama nguo na namna ambavyo amekua ni mtu wa kuninyanyasa, kunitukana kila siku. Uliniuliza kama anakupiga nikakuambia hapana.
Alijaribu siku moja nikampeleka Polisi hakurudia tena. Baada ya hapo uliniuliza swali ambalo naamini ndiyo limebadilisha maisha yuangu. Nakumbuka uliniuliza wakati mume wako anafanya yote hayo wewe unafanya nini? Sikukuelewa lakini ukaniambia wakati analewa anarudi usiku wa manane wewe nyumbani unafanya nini, wakati anakutukana na kuongea maneno ya kashifa wewe unafanya nini?
Nilikuambia nabaki nyumbani kumsubiri, nimelia nimechoka na akiongea mimi ni kulia tu. Ukaniambia, naongea na wewe, siwezi kumbadilisha mume wako lakini naweza kukubadilisha wewe, kama yeye kaamua kulewa hembu acha kulewa naye, acha kuumizwa na pombe zake, acha kumlea na pombe zake, acha kusubiria arudi, lala akirudi mfungulie na ikiwezekana mpe funguo.
Wakati yeye anatukana na kunyanyasa, wewe elekeza akili yako kwingine acha kuchukulia matusi yake siriasi na anza kumuona kama kondakta ambaye kila dakika anakupigia kelele kama unaenda Kariakoo wakati wewe unajua unaenda Ubungo. Acha kumsikiliza, akiongea wewe elekeza akili yako kwenye mambo ya maana, acha kuumizwa na maneno yake kwani hayakuhusu.
Hembu ishi kama single mother, uliniambia, badala ya kukaa kupoteza muda wako kutaka kumbadilisha hembu waza, hivi huyu mwanaume asingekuepo ningekua na fanya nini sasa hivi kisha fanya hicho kitu. Uliniambia soma sehemu ya nne na tengeneza furaha yako. Haikua rahisi Kaka, niliamua kukusikiliza, nilianza taratibu mpaka ikafikia hatua maneno yake yakawa hayaniumizi tena.
Akitukana chakula akinitukana maumbile yangu nilikua nacheka tu kichwani kwani wala nilikua nasikia kelele za Kariakoo wakati naenda zangu ubungo hazikunihusu. Nilianza kuwaza kama single mother, nikaweka malengo yangu mwenyewe, nikawa nafanya mambo yangu mwenyewe. Alipoona simfuatilii tena akaanza maneno tena kuwa nachepuka, nina mtu lakini bado sikujali.
Sasa hivi hata mwaka haujaisha tangu niamua kuwa kama single mother nimeweza kununua kiwanja changu, nimefungua biashara yangu wakati mwanzoni nilikua naogopa kwani alikua ananitukana kuwa siwezi chochote, siwezi kufanya biashara mimi ni hasara. Ninafuraha kwakua nimesema furaha yangu haimtegemei mtu mwingine, naona anataka kujirudi na kujishauashaua anataka nayeye kufungua biashara, namuangalia tu kwani haniumizi kichwa tena.
NB; Kama unatamani kusoma Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” Bei yake ni Shilingi elfu kumi tu. Kukipata unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222. Ukishalipia nitumie meseji ya Whatsapp au kawaida kwenye No. 0742-381-155 kusema unataka kutumiwa Kitabu kwa njia gani? Unaweza kutumiwa kwa Whatsapp, E-Mail au Facebook.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/nini-cha-kufanya-pale-mume-wako.html
No comments:
Post a Comment