Saturday, March 14, 2020

● OMBA UPENDO WA MOYO๐Ÿ’ž ● KATAA UPENDO WA MDOMO๐Ÿ‘…

Image may contain: 2 people, people smiling, people sitting and indoor

Mwanzo wa MAPENZI mtamu kama ASALI๐Ÿฏ muda wote Watu hujipamba kwa utamu wa penzi lao, Mwanaume akigeuka anaona ubora wa Mwanamke anajisemea HUYU NDIYE๐Ÿ‘Œ
Mwanamke akimtazama Mwanaume anajipa HOPE hakuna kama Huyu๐Ÿ‘
Siku hazigandi na kila mmoja kutarajia kwa yale aliyokuwa anayahitaji, Kila mmoja kusema mazuri na ubora kwa kumsifia Mwenza wake hata mashuhuda kujiuliza;
"WATU HAWA NI SPECIAL KWA NAMNA AMBAVYO WAMEPENDANA"
Kwa sababu Matendo ya MAPENZI yao yamebebwa na FURAHA MUDA WOTE๐Ÿ’ƒ
Muda nae ni rafiki wa kweli, Lakini Muda huyo huyo ni adui pindi mambo yanapokwenda ambavyo hukutarajia๐Ÿ˜ญ
Kinachoponza MAHUSIANO mengi ni MIHEMKO
Hakuna MALAIKA duniani sote ni bin adam ila kupitia changamoto mtu anaweza kujisahihisha na kuwa mtu mwema kuliko mwanzo, Mapenzi yakitawaliwa na MHEMKO maana yake fikra ya penzi inakuwa imeelemea kwenye uhitaji wa ki mwili kuliko maana halisi ya upendo, Urafiki mara zote umekomboa MAHUSIANO MENGI๐Ÿ’ช
Mahusiano mengi pamoja na ndoa za sasa zinapatikana kwa muda mchache, Wengi wanaanza kushiriki NGONO ndani ya siku 3, Wakinogewa wanapanga NDOA wakiwa kwenye mabanda ya juisi, Guest ama kwa njia ya simu, Na mikakati ya KUISHI PAMOJA inaanza mara moja, Wakati huo huo NDOA yao itakuwa imebebwa na MIHEMKO๐Ÿ˜œ
Mhemko hata Mimi ukinipata naweza kuacha kazi kumfuata Shemeji yenu na nipo nae kitambo JE WEWE AMBAYE NDO UMEKUTANA NA HALI HIYO UTAIKABILI VIPI?
Kwa sababu ukiingia kwenye MAPENZI kwa kufuata mhemko tafsiri yake ile kiu ikikata na UHUSIANO UMEKOMA๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
Jiulize sasa unahemka halafu ukakutana na Mwanamama anakwambia mpaka ndoa ndo univue๐Ÿ‘™maana yake inakubidi uchukue hatua ya UCHUMBA WA FASTER na bila kuchelewa NDOA itangazwe, Baba una "MSHOO" husikii la Mtu ni mpaka ukamilishe adhima yako, Ulivyo wa ajabu unaona ni UPENDO kumbe Mwili umekuponza
Baada ya muda PENZI TARATIBU LINACHUJA NA KUKOSA MUONEKANO ULE WA AWALI kila mmoja na kuanza kujutia, Muoaji alisukumwa na MHEMKO
Muolewaji nae aliona amepata, Basi kila mmoja kuugulia ki vyake Kwani tayari waliishajifunga, Chezea NDOA wewe hainaga mchezo, kuingia ni kwa SHEREHE ila ukitaka kutoka lazima SIMANZI IKUHUSU
Maisha yanahitaji utulivu wa akili ili kupata ufanisi ama vilivyo bora, Wengi wanarahisisha ili kukwepa changamoto huku wakisahau NO GAIN WITHOUT PAIN Kwani unaposumbukia kitu ni ngumu kukubari kipotee na ulishatumia muda, nguvu zako na Kuna wakati MALI ili kukipata.
MPE RAFIKI WA KWELI MOYO WAKO;
Rafiki wa kweli haumizi
Rafiki wa kweli hasaliti
Rafiki wa kweli atakupenda
Rafiki wa kweli hatakunyima muda wake
Rafiki wa kweli hawezi kukuhesabia makosa
Na ndipo unapata maana ya kwamba USIOLEWE NA MPENZI ila ikimpendeza MUNGU na akupe RAFIKI WA KWELI Kwani huyo atasimama na wewe nyakati zote, Mpenzi anaweza kukaa mbali pindi mtakapokuwa kwenye ugomvi, Lakini Rafiki wa kweli MUDA na AKILI yake vinakutazamia wewe na hawezi kukwepa MABADILIKO YA TABIA ZA KI BIN ADAM
Maana yake atakuwepo kuhakikisha kwamba HUPATI UPWEKE WA AINA YOYOTE na hilo ndilo linalobeba maana ya UPENDO WA DHATI
Ukiwa na Mpenzi peke yake ni ngumu kwake kukuelewa, Lakini uwapo na Rafiki wa kweli ni rahisi zaidi kueleweka na kubebewa madhaifu yako, Ukiwaona wana mahusiano ama wana ndoa wamedumu ujue kwamba URAFIKI ndiyo umewafikisha hapo, Wala usijisumbue kwa kuangalia MUONEKANO wa Mtu ila tafuta tabia yake kwa uhalisia kwa maana moja tu ANAWEZA KUWA RAFIKI MWEMA KWAKO haya mambo mengine wachana nayo YANAPITA
Raha ya uhusiano ama ndoa ni KUFURAHIA maana yake RAFIKI ndiye mwenye DHAMANA YA FURAHA wala sio MUME AU MKE hivyo ni vyeo tu ki mahusiano lakini pia ni UHALISIA WA KIJINSIA ๐Ÿ‘ซ
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria๐Ÿ”จ


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/omba-upendo-wa-moyo-kataa-upendo-wa.html

No comments:

Post a Comment