Monday, March 16, 2020

Mwanamke kataa kuwa MATEKA huku ukijua kwamba ukiisha kamatika itasemekana kwamba ULIJITEKA๐Ÿ˜Ž

Image may contain: 1 person, sitting and indoor
Mapenzi MATAMU NA MAZURI ni yale yanayo ongozwa na HISIA ila kama itatokana na ushawishi kwa sababu fulani basi wewe ni MATEKA TU๐Ÿ”ซ
Huwezi kudumu kwenye FURAHA ikiwa unapitia uhusiano ambao ni kwa ajili ya MATAMANIO๐Ÿšซ
Furaha inaweza kudumu na kuishi na Mtu ikiwa atampata Mtu ambaye yeye ANAFUATA HISIA ZAKE KWAKO lakini Kwa Maana moja tu UPENDO WA KUDUMU๐Ÿ’ช
Na kwa vyovyote vile MAPENZI yanahitaji kufuata misingi ya UPENDO ili kuwalinda wahusika, lakini ikiwa MAPENZI yenu yanaongozwa na faraja pamoja na vitisho vya JAMII inayo watazama, Kwamba MAPITO unayopitia inakubidi kuyavumilia kwa sababu Baba, Mama, Mjomba, Shangazi, Kaka na Dada ndio wanao kufanya uvumilie UNAJIDANGANYA na mwisho wako sio mzuri Kwani NI SAWA NA KUUMWA JINO UKALIMEZEWA DAWA YA KUTULIZA MAUMIVU ni kweli litapoa lakini ujue kwamba litakopoibua MAUMIVU itategemeana na hali itakayokuwepo ila DAWA YA JINO KUNG'OA๐Ÿ™‹
Huwezi kuambiwa VUMILIA wakati wao hawajui mateso unayopitia lakini pia unajikuta ukiwatazama wao waliyakataa mateso IWEJE WAKUPE MOYO KUKABILIANA NA MAMBO AMBAYO HAYANA UFUMBUZI๐Ÿšซ
Kosa sio kosa la awali pengine ni wakati wa kujifunza namna ya kutofautisha KUKOSEA NA KUJISAHIHISHA.
Lakini kosa ni kukosea ukasemehewa wala usiache kukosea kama ulivyokosea๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
MAUMIVU ya Mapenzi hayabebeki jilani, Ukiyabeba ni mzigo wa misumali kichwani, Jenga kujitenga na YAUMIZAYO MOYO ili uweke NURU usoni lakini pia NAFSI kutulia, Wasikudanganye YANA MWISHO wakati tangu umjue hujawahi ona nafuu, Kama wanaweza WAPE NAFASI NAO WAJARIBU.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria ๐Ÿ™‹


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/mwanamke-kataa-kuwa-mateka-huku-ukijua.html

No comments:

Post a Comment