Sunday, March 1, 2020

FURAHA HAINDOI MATATIZO, BALI NI UWEZO WAKO WA KUKABILIANA NAYO๐Ÿ’ช




Kwenye maisha yeyote yale MATATIZO ni sehemu ya kutambuwa badiliko la kile ambacho ulikitarajia ama ulichokiamini.
Watu wengi wamekuwa wakiyaona mahusiano yao kama sehemu ya MATESO wanayopitia kwa sababu wakati wanayaingia MAHUSIANO waliamini katika FURAHA wala hawakukumbuka juu ya UBIN ADAM na ndiyo Maana wanapoona tofauti wanakimbia na kwenda kuanzisha UHUSIANO mpya bila kujua chanzo cha yote hayo, Mwisho wa siku kila aendako anahisi hakuna tofauti na kumbe yeye ndiye chanzo cha MATATIZO๐Ÿ˜…
Furaha inazaliwa na Mtu mwenyewe, Hata kama FURAHA hiyo itatokana na Mwingine tambuwa wewe ndiye uliyeizalisha, Unakuta Mtu anahisi anadhurumiwa FURAHA YAKE KWA MTU AMPENDAYE ila yeye mwenyewe anasahau makosa yake yanayopelekea mwenza wake kukatika FURAHA aliyokuwa akimpa Mtu huyo, Ndo maana nikasema FURAHA HAITOWESHI MATATIZO kwa sababu ubin adam ni mahala pa kujifunzia mambo, Ukiona unayo FURAHA niamini wewe umeijenga FURAHA YAKO kwa sababu umekabiliana na yale ambayo yangemuumiza mwenza wako mngeingia kwenye MIGOGORO huo tayari ni USHINDI wako kuona kwamba uko na FURAHA lakini haitoshi uko na mtu anayekupa FURAHA ๐Ÿ’ƒ
Jifunze kujuwa kwamba HAKUNA MKAMILIFU DUNIANI ili uanze wewe kumfanya mwenzio awe mkamilifu ndipo uone vile anatakiwa KUKUPA FURAHA.
Jiondoe kwenye kujihesabia HAKI ama kuwa MBINAFSI hiyo itakufanya kumuona MWENZA wako ni mtu anayehitaji FURAHA ili akifurahi Basi na wewe uweze kufurahia, Lakini kama utapenda UFURAHI peke yako maana yake wewe ni KABAILA Yaani hutakaa umuone mjinga DUNIANI hata kama utamhonga mamilioni mwisho kabisa ATAKUJA KUKUACHA UBAKI UKINUNG'UNIKA๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
Raha ya MAHUSIANO ni kuweka UWIANO wa mapokeo ya UPENDO ili kila mmoja kuhisi FURAHA YA UWEPO WA MWENZA WAKE ๐Ÿ˜


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/furaha-haindoi-matatizo-bali-ni-uwezo.html

No comments:

Post a Comment