Sunday, March 1, 2020

Maisha sio; ▪PESA. ▪GARI. ▪NYUMBA.

Image may contain: 1 person
Bali maisha ni FURAHA NA AMANI hayo ndiyo yenye kuileta maana halisi ya KUISHI DUNIANI.
Kuna wenye vyote hivyo lakini hawana FURAHA WALA AMANI na kutwa wakililia kutafuta jinsi gani atapata FURAHA NA AMANI? Mwisho wa yote ni Mateso huku akiwa na kila kitu, Lakini aliye na Furaha na Amani hata akikosa kitu ni rahisi kwake kuyaona maisha ni mazuri tu, Kwa sababu FURAHA ni zao la MOYO na AMANI ni zao la NAFSI hivyo ndivyo vilivyo na mamlaka katika maisha ya kiumbe yeyote.
Kuna dhana mbaya sana WANAWAKE Mmekuwa na kiburi mnapokuwa na pesa kitu ambacho hakiwezi kukupa FURAHA WALA AMANI MILELE kama huamini ngoja nikupe ubuyu umung'unye๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 Unapata pesa unapata kiburi kwa sababu unajua unaweza kumpata Mwanaume yeyote umtakaye, Unaanza DHARAU kwa MUME ama MPENZI WAKO kisa unakutana na wanaume wanakusifia na kukupamba, Mama utasifiwa kila mtu atakuja na sifa yake mpaka hata ukijamba utapata mtu atakusifia NAPENDA MIJAMBO YAKO ili atimize malengo yake, Mwisho wa yote unabaki peke yako, Kutumia pesa ili kuwakamata wanaume haikomei kukuumiza wewe tu ila hata wanawake wenzio utawaumiza kwa sababu ndani ya wanaume unaopata kwa pesa zako Kuna waume za watu BIBI ACHA KIBURI CHA PESA Kwani kamwe huwezi kuiona FURAHA NA AMANI kwa sababu UPENDO NI MATENDO YA MOYO na pesa inabaki kuwa sehemu ya matumizi
Utampa pesa kwa mahitaji yake, Lakini MOYONI anae ampendaye hivyo ni wewe kubakia mjinga na wenzio wakifurahia MAPENZI YAO๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ
Kama unaona hupati FURAHA NA AMANI na Uko na Mume na pesa unayo jichunguze wapi ulikosea ili ujue kujisahihisha, FURAHA na AMANI vinaanza na wewe kwa kutimiza haja ya NAFSI yako ili MOYO upate kutulia, Vinginevyo UTATANGA NA NJIA WALA USIMUONE ATAKAYEKUELEWA kwa sababu kila atakayekuja atavutiwa na PESA ZAKO wala sio kwa UPENDO kama unavyodhania PESA yako ndiyo itakayomfanya awe nawe na mwisho kabisa ANARUDI KULE ILIKO NAFSI NA MOYO WAKE๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria๐Ÿ”จ


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/maisha-sio-pesa-gari-nyumba.html

No comments:

Post a Comment