Wednesday, June 17, 2020

Breaking News! TAARIFA MUHIMU KWA WASOMAJI WETU NA WATUMIAJI WA APP YETU YA UTAMU KITANDANI

International Breaking News - Home | Facebook

TUNAPENDA KUWATAARIFU WASOMAJI WETU KWAMBA TUMEPATA HITILAFU KWENYE APP ZETU ZILIZOPO GOOGLE PLAYSTORE HIVYO KUSABABISHA APP ZOTE KUONDOLEWA KABISA KWENYE MFUMO WA GOOGLE PLAYSTORE 
HIVYO TUNAPENDA KUWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAO JITOKEZA, KWA SASA TUNAJITAHIDI  KUFANAY MAREKEBISHO NA TUNAWAAHIDI 

KWAMBA MUDA SI MREFU APP YAKO PENDWA YA 
'UTAMU KITANDANI' ITARUDI TENA HEWANI NA UTAENDELEA KUFURAHIA KAMA ILIVYOKUWA ZAMANI

KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NASI KWA 0755542721
email ya kingazimediatz@gmail.com


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/breaking-news-taarifa-muhimu-kwa.html

Tuesday, June 16, 2020

ACHA KUWA KIAZI, MKISHAACHANA MMEACHANA HAKUNA KUACHANA VIZURI!


utamuzaidiapp
Dada zangu hembu jitambueni hata kidogo hivi mwanaume ulikua naye kwenye mahusiano, kakutumia wee kakuchakaza, mwisho kakuacha kaenda kuoa mwanamke mwingine. Baada ya muda anakuja kwako na kukuambia kakukumbuka, unakubali unamrudia, kila siku unagombana na mke wake bila aibu unamuambia “Wewe umeolewa lakini mimi ndiyo napendwa!” Dada, kwa taarifa yako hata magunia ya deki yanapendwa ila yanaishia kufutiwa miguu tu!
Kama alikuacha kipindi hana mke sasa hivi anarudi kwako kufanya nini? Ukiona mwanaume kakuacha, kaenda kuolewa na karudi kwako basi jua kuwa anakudharau! Anaona kabisa kuwa wewe huna maisha bila yeye. Lakini wakati mwingine hata hamkuachana kwa kuchokana, hapana, mwanaume mlikua mnapenda, labda mkaachana kwasababu ya Dini au Kabila, wazazi hawataki, lakini nyie bado mnapendana.
Ameenda kaoa anarudi mnaendelea naye, aisee hakuna kitu kinapoteza muda kwa mwanamke kama kuendelea kufanya mapenzi na X wako ambaye mlikua mnapendana. Dada zangu, mwanaume mkiachana bila kujali sababu za kuachana basi kata mawasiliano naye, yaani hata akifa msiba wake usipost, achana na haya mambo ya hatukuachana vibaya, aisee inaharibu maisha yako.
Inawezekana kweli anakupenda kuliko mke wake, lakini yule ni mke. Inawezekana kuwa anakujali ila kama hamkuoana basi hamkuoana, yaani hamtakuja kuoana. Umekaa hivyo, baada ya muda unashangaa una miaka 40, mwenzako bado ni mume wa mtu, anafamilia yake, umemsaidia kafanikiwa, ana maisha yake, ila kumbuka hayo mafanikio ni ya wewe na mke wake. Itakula kwako acha huo ujinga, aisee, kuendelea kuwasiliana na mume wa mtu kisa wewe ndiyo unapendwa wakati alikuacha na kuoa huo ni UKIAZI!
Nishamaliza ila kasirikeni basi hata muache!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/acha-kuwa-kiazi-mkishaachana-mmeachana.html

USIUDANGANYE MOYO WAKO KWAMBA ULIYE NAE MNAENDANA KISA ULIPENDA UWE NA MWENZA ALIYE SMART KESHO NI FUMBO πŸ€”


Muonekano unaweza kupotea kwa hali ya maisha kubadilika ama ugonjwa na wakati mwingine umri nao ni sehemu ya badiliko la MUONEKANO.
Unaweza kuamini kwa macho lakini ikawa sio vile NAFSI YAKO INAHITAJI na tatizo limewapata wengi, Unamtazama Mtu na kuamini kuwa ni yeye pengine ni kwa sababu tu ana sifa mbili kati ya zile ulipenda awe nazo MWENZA WA MAISHA YAKOπŸ’‘
Haja ya nafsi haitafutwi kwa majaribio, lakini pia kumbuka wazi ULIVYO LEO UNAWEZA KUWA BORA ZAIDI BAADAYE ukajikuta unamuona mwenza wako haendani nawe tena na hapo utanielewa nikisema MUONEKANO WA MTU SIO HITAJI LA NAFSI ila ni ukosefu wa utulivu wa HISIA ZAKO.
Mchukuwe Mtu aliye chaguliwa na NAFSI YAKO halafu mjazie mapungufu yake, Mfanye awe kamili kama ulivyohitaji Mwenza wako awe, Ndo maana ni rahisi kwa Mwanaume kuwa na MWANAMKE WA NAFSI YAKE kuliko Mwanamke kuwa na Mwanaume wa NAFSI YAKE sababu ni ndogo sana:-
 Mwanaume kumuoa Mwanamke na kwenda kumtengeneza ni rahisi, kuliko Mwanamke kuchukuwa Mwanaume wa HISIA zake na kwenda kumtengeneza, Kwani tamaduni zetu zitamfanya Mwanamke huyo kuonekana ANAMHONGA MWANAUME wakati huo Mwanaume kumhudumia Mwanamke ni wajibu hata vitabu vya dini vimeagiza hilo.
Kwa sababu hiyo WANAWAKE wengi wanaolewa na wanaume wasokuwa wa NAFSI ZAO kwa sababu pamoja na Mwanamke kupenda Mwanaume SMART lakini pia kumkuta Mwanaume ameji-bland mwenyewe ni USHINDI Kwani Hawa viumbe nao UNAWEZA KUMTENGENEZA ukanyanganywa na SHOST πŸ˜‚πŸ˜‚
Halafu Mwanaume HAFUGIKI kama hujui Jaribu KUMFUGA UJE KULIA🀸‍♂️🀸
utamuzaidiapp


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/usiudanganye-moyo-wako-kwamba-uliye-nae.html

Ijue tofauti kati ya UPENDO WA MWANAUME NA MWANAMKE;


 Mwanaume akimpenda Mwanamke anamuweka akilini, yaani kama kuna VIONJO VIPO KI PEKEE atadumu nawe akilini mwakeπŸ˜‚ na wenye BAHATI wao mpaka moyoni huzama hao ndo humfanya Mwanaume hata KUJIUA kulikosa penzi la Mwanamke aliyempenda.
 Mwanamke akimpenda Mwanaume ANAMUWEKA MOYONI wala hapatakuwepo na Mwanaume mwingine ataweza kukuondoa hata awe na NGUVU GANI kwa hakika hataweza kumuingiza MOYONI ila ataweza kumuingiza akilini kwa SABABU ZA KI MAISHA.
Mpaka hapo ushajua kwanini MAPENZI YANA RUN DUNIA🌎
Kila MBABE NA MBABE WAKE πŸ˜‚ ila ukiona wewe unaonewa na Mtu umpendaye ujue kuna mahala nae ni FALA TU πŸ€£πŸ€£ anapelekeshwa mpaka mwishooo, Ndo maana halisi ya UPENDO πŸ’ž UPOFUπŸ€”
Mheshimu akupaye AMANI YA MOYO πŸ’– vinginevyo utajitafutia MARADHI BURE πŸ€¦‍♂️
Maana UTULIVU WA NAFSI UNATOKANA NA HITAJI LAKE kinyume chake utalazimisha kusahau kisichosahaulika mwisho kabisa UFE UNAJIONA πŸ˜­πŸ˜­
utamuzaidiapp


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/ijue-tofauti-kati-ya-upendo-wa-mwanaume.html

MWANAUME ANGEMPENDA MWANAMKE KWA MOYO πŸ’– WAKE WALA ASINGEACHA KURIDHIKA NA MWANAMKE MMOJA ⛔


Mwanaume ni sawa na mgonjwa wa kisukari πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Yaani ni kweli AMEOAπŸ‘©‍❤️‍πŸ‘¨ ila kuacha kupata hamu kwa Mwanamke mzuri zaidi ya mkewe ni kama DHAMBI🀦‍♂️
Ndo maana nikamlinganisha Mwanaume na mgonjwa wa kisukari, ni kweli ametakiwa kuacha vitu vitamu ila akiona FANTA anameza mate πŸ˜‹
Tatizo sio UZURI WA MWANAMKE  tatizo kubwa linawapata wanaume ni KUTOMKUBARI MWANAMKE ALIYE NAYE na kuamini katika FARASIπŸ¦„ UKIMPANDA HAKUTISHI MIONDOKO wakati huo huo MWANAMKE aliyemfanya amdharau aliye nae kuna Mwanaume kamkinai hapo ndipo utanielewa TATIZO LA WANAUME SIO UZURI WA MWANAMKE  tatizo lao kuu KIUπŸ˜‚πŸ˜‚
Muda wote wanatamani kuonja kila KISIMA bila hata kujua wataleta MADHARA gani kwa aliyepoπŸ€”
Visima vingine ukionja maji yake utahamia na hapo ndipo utanielewa kwamba KULIKO KUONJA ONJA CHIMBA KISIMA CHAKO MWENYEWE🀝
utamuzaidiapp


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/mwanaume-angempenda-mwanamke-kwa-moyo.html

USICHELEWE KUMUONYESHA UPENDO WAKO WA DHATI πŸ’• YULE ALIYEANDIKWA NAFSINI MWAKO⛔


Kuna wakati upendo huo utakuwa hauna maana tena baada ya MAUMIVU MAKALI ULIMPITISHA NAYO akiamini huna UPENDO WA DHATI πŸ’• KWAKE.
Na ndipo utajua ni kiasi gani inauma ikiwa UNAMPENDA MTU LAKINI HAJUI😭
Maumivu yale aliumia MHITAJI hugeuka kuwa MAUMIVU YAKO na hapo ndipo utanielewa kwamba kuliko KUUFICHA UPENDO kwa kuogopa akijua UNAMPENDA atakuona wewe ni DHAIFU na huo ndo ujinga kweli kweli maana UDHAIFU NDIYO HUONYESHA UPENDO WAKO KWA MTU kwa kuuficha UDHAIFU wako tarajia kuonekana huna UPENDO WA DHATI πŸ’• na mwisho kabisa ni wewe kubakia MPWEKE kwa uzembe wako😭
Onyesha UPENDO WAKO WOTE KWA YULE ULIYEMPENDA ili upokee AMANI moyoni mwako, Kumkosa uliyempenda ni HATARI sana lakini pia ni rahisi kukosa wa kumpenda duniani Kwani UPENDO WA KWELI NI KWA MMOJA ❤️
Usijidanganye kuna mwingine ataleta MAPINDUZI NAFSINI MWAKO baada ya yule uliyempenda kuondoka maisha mwako, zaidi utaishi kwa Mahangaiko ya NAFSI kwa Kumkosa ULIYEMPENDA huku ukileta mateso yale yale kwa uliyedhani ndiye AMEZIBA NAFASI YA ALIYEONDOKA 
Nafsi inabeba mmoja, Mwingine atakuwepo kwa sababu zako nae akijua HUMPENDI ataondoka na akibakia atakuwa na sababu ya kubaki na hiyo ndiyo italeta maana ya KUBAKIA KWA SABABU NA MANUFAA YAKEπŸ€”
Mapenzi ni MATAMU BANAAA πŸ˜‹ hasa ukiwa na ULIYEMPENDA KWA DHATI YAKO maana kupitia upendo wako nae ATAKUPENDA Kwani UPENDO HUISHI NA UPENDO πŸ’ž
Ukiona HUMPENDI mtu nawe tarajia HATAKUPENDA Yaani MOYO πŸ’– Una sikia kwenye UPENDO WA KWELI ili kama ukiona hupendwi basi ulishiriki kutopendwa, Tafuta uwiano wa UPENDO πŸ’˜ WA DHATI kwa kumpenda mwingine ✔️
Image may contain: 2 people, people standing, tree and outdoor


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/usichelewe-kumuonyesha-upendo-wako-wa.html

MWANAMKE ANAPOUMIA HAIMFANYI ASIPENDE TENA KWA SABABU KWAKE KUPENDA NI WITO JAPO TATIZO NI NAMNA GANI ATAAMINI BAADA YA KUUMIZWA🀷‍♂️


Maisha ya Mwanamke huchanua tangu angali msichana, namna nzuri ya kuamini juu ya UKOMBOZI WA MWANAMKE NI BAADA YA KUJENGWA KATIKA MSINGI WA KUJITEGEMEA MWENYEWE.
Familia zilizo nyingi zinamjenga BINTI katika kuiheshimu NDOA hata kama itakuwa haileti UKOMBOZI MAISHANI MWAKE na hilo ndilo anguko kubwa la maisha ya Mwanamke πŸ˜­πŸ˜­
Mwanamke akiishi kwenye mafunzo ya kuiabudu NDOA basi hata awe mwenye ELIMU kubwa kiasi ATAISHI KAMA MTUMWA.
Mwanamke akijikomboa ki fikra kamwe hataishi kwa kuogopa:-
 JAMII.
 MUME.
 DINI.
 MWANAMKE MWENZIE.
Mwanamke aliyejikomboa kamwe hataangalia DUNIA ITASEMA NINI bali atakuwa YEYE na wala hataruhusu KITU AMA MTU aingilie UHURU WA NAFSI YAKE 
Wanawake wengi wameangamia kwa kuangalia DUNIA ITASEMAJE na kujikuta wameangukia kwenye NDOA zilizojeruhi maisha yao yote, Kila kukicha anashukuru MUNGU na kujisemea siku moja MUNGU ATALETA MUUJIZA KWAKE huku akisahau anguko lake lilijengwa na MALEZI YAKE😭😭
Elimu ya mzazi kwa binti yake hiyo inaweza kuleta UKOMBOZI ama UHARIBIFU wa Maisha yake, Kwa sababu ikiwa BINTI atajengwa katika msingi wa KUOGOPA JAMII kamwe hataona:-
 VIPIGO.
 FEDHEHA.
 UDHALILISHWAJI.
Mbaya zaidi anaweza kusoma vitabu vitakatifu akajua AGIZO LA MUNGU KWAKE NA KWA MUMEWE lakini hataweza kubaini kosa la yeye KUMLEA MWANAUME ambaye aliagizwa kula kwa jasho, KUTAFUTA kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, Hali hiyo itatokana na WOGA WA KUACHIKA etiiii DUNIA isimchekeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/mwanamke-anapoumia-haimfanyi-asipende.html

Mwanaume na Mwanamke usikose URAFIKI WA MAPENZI

Mwanaume na Mwanamke usikose URAFIKI WA MAPENZI:-
"boyfriend and girlfriend" kabla ya NDOA yako.
Urafiki kabla ya ndoa huo ndiyo huibua TABIA HALISI YA MTU kwa vyovyote vile hupashwi kuingia kwenye ndoa kama hujawa na utambuzi wa tabia ya mwenza wako, Watu wengi wamejikuta wanaugulia MIOYO YAO baada ya wenza wao kutokuwa kama walivyo watarajia, Unajua kuna mambo mawili tofauti ila wengi hawajui kutofautisha ni kati ya;
 MAKOSA.
 UDHAIFU.
Makosa yana eneo lake ambalo ni baada ya Mtu kujikuta kakosea iwe kwa kujua ama makusudi lakini akajua kwamba hakupashwa kufanya hivyo, Udhaifu ni ama uhalisia wa Mtu au ni kutokana na kushindwa kuhimili changamoto.
Imagine unaingia kwenye ndoa na Mtu ambaye hujui madhaifu yake unajua unaweza kujua ni MAKOSA wakati ndo udhaifu wake,
MFANO;
Humjui mtu, Mmekutana ukitokea kwenye Mahusiano aliyoyapenda ila yakamuumiza, na wewe umeachwa ama kumuacha uliyempenda na nyote kila mmoja akitafuta FARAJA unafikiri atakuacha uende zako wakati anahisi wewe ni rafiki mzuri πŸ€·‍♂️
Mtu anayetaka FARAJA HAAMINIKI  na ukijaribu kumuamini kuna wakati utakuja KUKULIZA wala hutaamini, Still analo pendo la dhati kwa aliyemuumiza, Kwa sababu hatuwezi KUUMIA kwa watu ama kitu usichokipenda, Mara zote UNACHOKIPENDA ndicho huleta maumivu baada ya HITAJI LA NAFSI KUKOSEKANA πŸ˜­πŸ˜­
Kwa maana hiyo, Aliyeumizwa haimaanishi anataka MTU MWINGINE  ila anataka RELIEF huku akiendelea kubembeleza arudiwe ama asamehewe kwa makosa aliyokosa, Ni ngumu sana KUMPATA MTU ALIYE HURU MOYONI ila ukimpata huyo MSHIKE πŸ€ kwa sababu huyo ataleta MAPINDUZI NAFSINI MWAKOπŸ‘
Nature ya MOYO πŸ’ž haubebi wawili ila MMOJA sasa kama unajua umeingia kwenye UHUSIANO/NDOA ya mtu aliyempenda mwingine niamini UNAKUWA NA NAFASI NDOGO MNO MOYONI MWAKEπŸ€”


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/mwanaume-na-mwanamke-usikose-urafiki-wa.html

WANAWAKE WENGI WAKISHAOLEWA HUDHANI MAISHA YAMEISHA, WANAJISAHAU.


utamuzaidiapp

Wanawake wengi wakishaolewa hudhani kuwa maisha yameisha, wanajisahau kwa namna flani, ile dhana kuwa mwanaume yupo basi inawachanganya sana, inawaondolea ule mzuka wa kutafuta, ile hamu ya mafanikio, hasa wale wanawake ambao waume zao wanajali, wanahudumia kila kitu. Wanawake kama hawa wanajisahau sana katika suala la kutafuta, hawa ndiyo utasikia;
(1) Nasubiri kwanza nimalize kuzaa ndiyo nitafute kazi au nifanye Biashara; Ukweli ni kuwa mume anahudumia sina haja ya kubeba mimba huku nikifanya kazi!
(2) Mimba yangu inanisumbua siwezi kufanya chochote; Nikweli wakati mwingine mimba sinasumbua, lakini wanaacha kazi kwakua kuna anayehudumia, single mother angekomaa na bosi na maruhusa, angehangaika na mabarua mpaka basi, single mother asingefunga Biashara, angeajiri mtu lakini kila siku angefuatilia, simu zingepigwa mpaka basi.
(3) Nasubiri mpaka mtoto akue, wanangu hawawezi kulelewa na Dada wa kazi! Wadada wa kazi siku hizi kupata shida; Hapo unakuta mtoto ana mwaka mmoja, sijui anasubiri akue mpaka awe daktari au, hakuna kasi sana ya kutafuta dada wa kazi kwakua hana haraka ya kutafuta kazi, angekua single mother mtoto angebeba hata mgongoni afanye kazi.
Dada yangu, acha kujisahau, anza sasa, anza na kitu kidogo ambacho kinawezekana kwako.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/wanawake-wengi-wakishaolewa-hudhani.html

USHAWAHI KUKUTANA NA WALE WADADA WANAOUZA BIRIANI PEPONI?


Hakuna wanawake ambao wanajisikia raha kama wale wanawake ambao anatembea na mume wa mtu, halafu mwanaume anamshirikisha kila kitu. Mwanaume hawezi kufanya kitu cha maendeleo, iwe ni Biashara au kujenga bila kumuambia na kutaka maoni yake.
Wanajiona sana aisee, yaani ukiwasikia wanavyojisifia kuwa, ananipenda kuliko mke wake, mke wake hana akili,a lifunguliwa duka akalila lote. Basi unaweza udhani ni wale wadada wa peponi amabo wanapika Biriani kila Jumanna (Biriani la kule ni Jumanne).
Hasa ukute mke wa jamaa ni Mama wa nyumbani aisee watasumbua mpaka basi. Lakini ukweli nikuwa hakuna wanawake VIAZI kama hawa. Yaani tena ni vile viazi ambavyo unakuta vimetobolewa, ukikipika unakuta ni kichungu. Wako vizuri na wana akili ya kutafuta, wana mawazo mazuri lakini ni viazi kwenye mapenzi. Najua washaanza kutoa povu kuwa Kaka iddi anatukana hivyo ngoja niwakumbushe tu kidogo.
(1) Anakuambia anakupenda na una akili kuliko mke wake. Mawazo yote ya baishara unatoa wewe, lakini biashara zake na nyumba zake zote zina majija yake. Akifa mke wake mliyekua mnamuona mjinga ndiyo anarithi na wewe unarudi kulia ndani na akili zako.
(2) Mwenzako kaoa, anakuambia anakupenda hampendi mke wake, lakini hamuachi,a nabaki naye hivyo hivyo. Anakubana hataki uwe na mtu, watu wa kikutongoza wanasikia unetembea na flani wanaondoka, ukija kushtuka umri umeenda unaanza sasa kufunga, kusali kila siku,ili kutafuta mume wakati mwenzako anamaisha yake yanaendelea.
(3) Nishamaliza kama hizo sababu hazijakutosha, basi nunua Kitabu changu, nipigie nikupe appointment uongee na mimi, uje nikuambie acha ukinga. Nikuambie namna atakavyokutapeli. Ila kama huniamini hembu fanya hivi, sasa hivia kija kukuomba mawazo ya baishara muambie unataka muwe shea majina yenu wawili na kama ni nyumba muambie kiwanja aandike jina lako uone kama hatakimbia!
utamuzaidiapp


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/ushawahi-kukutana-na-wale-wadada.html

Monday, June 15, 2020

UNAUSHUHULIKIAJE MOYO ULIOUMIZWA??


Tunaumizwa ktk mazingira tofauti sana
Tunaofautiana namna ya kuumia na hali ya kukabiliana na maumivu
Inauma zaidi ikiwa aliyekuumiza ni mtu wa karibu na wewe
Unafanyaje???
1. Jitie moyo kwamba utavuka tu
2. Ongea na mtu anayejali, usijifungie au kuficha. Mwone mshauri ikibidi
3. Wewe ni binadamu ruhusu maumivu na machungu, usiyafiche au kuyakataa. Muda huponya.
4. Kama unaimani, peleka moyo wako uliyoumia kwa Mungu wako. Omba ila usilalamike
5. Jipe muda wa uponyaji (acha kuvuta hisia za mumivu)
6. Jifunze kitu kwenye tukio zima
7. Tafuta kitu cha kushukuru au kuwa positive hata kama ni kidogo
8. Kama kuna cha kusamehe basi samehe na achilia
Mtu wa kwanza mwenye mchango mkubwa wa kukutoa hapo ulipoumizwa ni wewe mwenyewe #
UTAMUZAIDIAPP


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/06/unaushuhulikiaje-moyo-ulioumizwa.html