USIOGOPE KUMPOTEZA MTU AMBAYE MALENGO YAKE KWAKO YALIKUWA NI MAMBO YA KUFIKIRIKA;
▪ HAJA YA MWILI
▪ MISAADA
▪ MATUMIZI
Na mambo ambayo yanatokana na KUPEANA.
Bin adam alipewa kipawa cha kufikiri na ndo maana ya UBIN ADAM WAKE Kwani nae ni kiumbe kama alivyo MBUZI🐐
Viumbe wote wanashiriki mambo tufanyayi bin adam except MAPENZI ila kwa aina ya kiumbe husika, Lakini BIN ADAM alipewa upendeleo kutokana na UTAMBUZI WA MEMA NA MABAYA
Kuogopa kuachwa na Mtu ambaye yeye kwako alikuja kwa mtazamo wa NGONO ama KUTIMIZA MALENGO YAKE ni Sawa na kujitazama kwenye kioo halafu ukajizomea😅
Ogopa kuondokwa na Mtu ambaye alishiriki nawe kwenye FURAHA, MAJONZI lakini pia aliguswa MATESO YAKO
Mtu alijua kwamba UWEPO WAKO KWAKE NI AMANI YA MOYO WAKE huyo ndiyo wa kuogopa asisogeze mguu wake japo hatua moja, Huyo ndiye anaweza kuumiza moyo wako na ukateseka kumpata wa kufanana nae na ni ngumu mno KUMUONA TENA WA UHALISIA WAKE.
Mtu aliyekuja kwako kwa TAMAA ZAKE BINAFSI anakukosesha usingizi? Kweli MAPENZI yanauma ila sio kwa Mtu ambaye uliposema UNAUMWA alikupa kisogo, Sio kwa Mtu ambaye uliposema HUJISIKII alikuweka pembeni.
Umia kwa Mtu ambaye kila ulipoonyesha hauko nomal ALITAMANI KUKUREJESHA KWENYE HALI YAKO
Umia kwa Mtu ambaye alipohisi umekata tamaa HAKUTAKA AWE MBALI NAWE
Umia Kwa Mtu ambaye alipoona chozi lako ALISIKIA HURUMA
Umia kwa Mtu ambaye alipojua kwamba uko kwenye matatizo ALISHIRIKI IPASAVYO
Huyo ndiye hata mjinga atajua UMUHIMU WAKE ila sio kwa Mtu ambaye alipenda MPISHANO WA MAPAJA na ulipomwambia MWEZI UMEANDAMA ALISEPA BILA KUJIBU HATA MSG maana tayari MTELEZO umeingiwa TOPE.
#Elista_Kasema_ila_Sio_She
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/usiogope-kumpoteza-mtu-ambaye-malengo.html
No comments:
Post a Comment