Monday, March 16, 2020

HIVI UNAJUA UMUHIMU WA MSAMAHA NA KUOMBA MSAMAHA

Image may contain: 2 people

Msamaha ni tendo la MAJUTO kwa kile ambacho hakikutarajiwa kutokana na IMANI ama ni kilichotarajiwa kunusuru simanzi moyoni mwa aliyekosewa๐Ÿ™‡
Kukosea ni sehemu ya kujifunza makosa yasotakiwa kufanyiwa mwingine, Ama ni kile ambacho mtu baada ya kujua kosa lake ndo maana anaamua kukiri na kusema hawezi kurudia kosa, Japo kuna Mwingine anaweza kutumia mwanya wa msamaha ili kuhalalisha maana ya alichokosea, Pamoja na yote haina maana kung'ang'ania hasira kwani ni kujibebesha mzigo usokuwa na sababu kuubeba, Lakini sio kila mkosaji anapashwa kusamehewa, Maana majibu ya msamaha yanalenga KUSAHIHISHA KOSA ila utambuwe kuna kusamehe ukasababisha mkosaji kujenga TABIA ama ukasemehe na ukamkomboa mkosaji๐Ÿ˜…
Unaposamehe UNAJIFUNGUA KUTOKA KWENYE LINDI LA MAUMIVU๐Ÿ’†
Kubeba Makosa ya Mtu ni mzigo Sawa na kubeba MISUMALI kichwani๐Ÿ˜‚
Panaposameheka SAMEHE NGW'ANA WANHE ili maisha yaendelee, Kujaribu kukataa uhalisia wa kosa ni sawa na kukataa kwamba HAKUNA MAISHA BAADA YA MAUMIVU
Usitamani UGOMVI bali Jenga ngome ya AMANI kwenye UHUSIANO WAKO ili ujitenge na MAKWAZO
Msamaha una NGUVU๐Ÿ’ช๐Ÿฝ ya kusahaulisha yaliyokuumiza, Na kama kweli mkosaji atajua kosa lake basi MSAMEHE ila kama Mtu haongelei kosa lake na anataka msamaha HUYO ANATAKA KUKUNYAMAZISHA KWA WAKATI HUO niamini baadaye atarudia kosa kama alilokukosea, Usahihi wa MSAMAHA NI KUTUBIA KOSA kinyume chake ni DHARAU.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/hivi-unajua-umuhimu-wa-msamaha-na.html

No comments:

Post a Comment