Monday, March 16, 2020

HARUSI NI SHEREHE KAMA ZILIVYO SHEREHE ZINGINE๐Ÿ’‘

Image may contain: 7 people, people smiling, wedding and outdoor
NDOA ni TENDO la NAFSI wala haina maana kwamba chakula, vinywaji ama mziki๐Ÿ“ฏ๐Ÿ“ข mnene pamoja na mavazi ya aghari๐Ÿ‘˜๐Ÿ‘ ๐Ÿ‘œ๐Ÿ‘–๐Ÿ‘•๐Ÿ‘” kukodi magari ๐Ÿš˜๐Ÿš— ya fahari ndo iwe sababu ya kuilinda AMANI YA NDOA YENU๐Ÿšซ
NDOA ni agano๐Ÿ“– la MUNGU kwa watu wake, Kwamba baada ya KUZALIWA๐Ÿ‘ช ni KUOA AMA KUOLEWA na baadaye KIFO lakini lililo la taabu kati ya hayo ni KUOA/KUOLEWA๐Ÿ‘‚
Wengi wamekuwa na shauku ya NDOA kufurahisha jamiii pamoja na FAHARI YA MACHO pengine utazamapo picha jinsi ulivyovyaa ukapendeza, Nguo za HARUSI wala haziwezi kuijenga NDOA yenu Kwani NDOA hujengwa kwa MATENDO YA MOYO WA MTU.
Ni bora NDOA inayojengwa kwa UTASHI kuliko NDOA inayojengwa kwa SHEREHE kwa sababu sherehe haidumu bali UTASHI UNAISHI NDANI YA ALIYETAJWA KUWA NAO.
SHEREHE hudumu kama KUMBUKUMBU TU wala huwezi kuilinda SHEREHE ikaishi nawe maishani mwako ikiwa MWENZA wako hakuja kwako kwa mtazamo wa KUILINDA SHEREHE YENU IKADUMU NA KUIJENGA FURAHA SIKU ZOTE hata hapo kifo kitakapo watenganisha, Kuilinda AHADI YA NDOA ni rahisi kwa mtazamo wa wana ndoa wenyewe lakini pia KUIBOMOA AHADI YA NDOA NI MTAZAMO WA WANANDOA WENYEWE.
Ndoa hulindwa kwa maana ya NDOA wala huwezi kutenganisha UAMINIFU KWENYE NDOA kwa sababu UAMINIFU ni msingi imara kwa wawili waloamua kuwa WAMOJA.
Usiparamie SHEREHE ili kukupa FURAHA kwamba uliolewa, Mbona inawezekana waliobebana bila SHEREHE wakawa na AMANI kuliko wanaopitia HONEY MOON.
Wana ndoa wengi MAPENZI YAO HUISHIA HONEY MOON pale tu wanapotakiwa kuwajibika ili kuileta maana ya NDOA yao hapo ndipo UFA HUANZIA๐Ÿ˜ญ
Kwa sababu kwenye UHUSIANO wa kawaida UONGO NA MATUMAINI hutawala ili kusababisha kumlinda mwenza asikuondoke, Lakini ujinga ni kwamba MTU KUAMINI NDOA "pete na viapo madhabahuni" eti ndo siraha ya kuona hamuwezi kuachana, Kuachwa kuko pale pale kwa sababu kila mtu hukubari awe na mtu ili KUUTETEA MOYO WAKE KWAMBA AMANI YA NAFSI ITAWALE ila kama hayo hayapo wala usijidanganye kwamba NDOA ndo kitanzi labda kwa mjinga asojua maana ya AMANI NA FURAHA.
Kabla ya NDOA jichunguze kama unakwenda kwenye NDOA kwa kuimaanisha maana ya NDOA๐Ÿ’ช
Ingia kwenye NDOA ili kwenda kuitetea NAFSI yako lakini pia KUMLINDA MWENZA WAKO! Kinyume cha hayo ni wewe kuwa MHANGA WA NDOA lakini pia MWENZA WAKO KUMUUMIZA.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/harusi-ni-sherehe-kama-zilivyo-sherehe.html

No comments:

Post a Comment