Friday, March 13, 2020

USIMCHUNGUZE MTU UNAYE AMINI YUPO KWENYE SAKAFU YA MOYO WAKO๐Ÿ’ž

Image may contain: 2 people, selfie, phone and close-up
Mapenzi IMANI japo usijiamini wewe mwenyewe, Kuwa na IMANI YA UHUSIANO ULIOPO
Inaweza kuwa dawa nzuri kwenye AMANI YA PENZI HUSIKA. Wivu ni kiashiria cha UPENDO kwamba Mtu analilia uhakika wa penzi lake, Lakini usiwe mchunguzi wa kutaka kujua ambayo yako nyuma ya PAZIA.
Kwa sababu unaweza kuona jambo ama kusikia ukalipa mtazamo ambao sio kwa uharibifu wa penzi lako pengine ni katika kujenga DHAMANA YA PENZI
Kila mwana wa adam ni DHAIFU kwamba hakuna aliye mkamilifu, Uliwahi kuujua UDHAIFU WAKO MWENYEWE? Hakuna ajuaye udhaifu wake ila kupitia wengine unaweza kujua baada ya kufanya jambo ambalo litasababisha kuonyesha udhaifu wako.
Ikiwa udhaifu wako huwezi kuujua IWEJE KUTAKA KUUJUA UDHAIFU WA MWENZAKO?
Mtu hawezi KUCHUNGWA lakini unaweza KUMKUMBUSHA KUJIHESHIMU zaidi ya hapo ni kumnyima UHURU BINAFSI kwa sababu MAPENZI YAKIKOSA UHURU husababisha CHUKI kwa maana hiyo jenga utamaduni wa kumkumbusha Mwenza wako; MNATOKA WAPI?
MKO WAPI?
MNAKWENDA WAPI?
NINI MAANA YA UMOJA WENU?
ili ajue pengine unaona mwenendo wa penzi lenu hauko kwenye MSINGI WA MAKUTANO YENU ni pamoja na kumwambia juu ya HESHIMA YAKO KWAKE.
Kwa sababu Kuna watu akiishaingia kwenye UHUSIANO anajiona yeye ndiye yeye, Matusi, dharau, kebehi, usaliti na mengineyo yanayoumiza MOYO wala asijue MAUMIVU YAKO.
KWANINI USIMCHUNGUZE?
Usimchunguze kwa sababu ni ngumu kutomkuta na TATIZO je upo tayari kukabiliana na hali iyakayokujia? Kuliko kujitesa na mambo ya kumchunguza Basi FUATILIA MIENENDO YAKE TU ili ubaini mabadiliko aliyonayo kwa wakati huo bila hata kutafuta kiini chake, Kwa sababu ni MTU MZIMA iweje asijue kama kwa kufanya kinyume na alivyokuahidi ni kosa?
Mtu akibadilisha mtazamo wala usisumbuke kujua njia zake ila ninaloweza kukushauri ni kwamba;
"FIKIRIA ZAIDI KUWA NA AMANI KULIKO KUITAFUTA AMANI"
Lakini pia nikukumbushe kwamba USIRI WA SIMU ni chanzo cha YALIYOKO NYUMA YA PAZIA Yaani Mtu ana password kama zote kwenye simu BADO ANAKWAMBIA NAKUPENDA UNAKUBARI?
Hakuna siri ngumu kuonwa kama UTUPU sasa kama anajua mpaka BUSTANINI halafu anakuficha simu unajipa hakika kwamba UPO MWENYEWE?
Kumuua nzi sogea eneo lenye HARUFU Mbona hutasumbuka, Wala usijitaabishe kumjua MUONGO ni MIENENDO YAKE TU.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria๐Ÿ˜Ž


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/usimchunguze-mtu-unaye-amini-yupo.html

No comments:

Post a Comment