Monday, March 23, 2020

UNAWEZAJE KUJENGA DHAMANA NDANI YA MOYO WA MWENZA WAKO?

 
Image may contain: 2 people, people smiling, people standing and outdoor
Kwanza kabisa ujue MAPENZI NI MAISHA na ili uweze kuyaishi Mpenzi ni jukumu lako kusimamia Misingi ya penzi husika, MUDA ni sehemu ya Mapenzi kadiri unavyoweza kumpa Muda wako mwenza wako ni wazi unajenga dhamana moyoni mwake, AKILI ni sehemu ya utambuzi wa mambo yako hivyo ni vizuri kujua umuhimu wa mwenza wako na hilo litamjenga mwenzio kukupa dhamana, MWILI ni ushuhuda wa matendo yahusuyo Mapenzi kwa vyovyote vile muingiliano wenu unajenga dhamana ya penzi lenu, KUJITOA ni eneo linaloweza kumfanya Mwenza wako akajiona unamthamini na hilo litampa sababu ya kukupa dhamana ya pekee moyoni mwake, Hayo ni mambo makuu kuijenga BOND kwa mwenza wako, Ukimpa MUDA atakupa MUDA... Ukimpa AKILI nae atatumia AKILI kuishi nawe, Ukimpa MWILI atakupa MWILI mtaunganisha joto lenu, Ukiweza KUJITOA kwake niamini ATAJITOA! Kwani nature ya MAPENZI NI KUAMBUKIZANA YALE YAUFURAHISHAYO MOYO.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/unawezaje-kujenga-dhamana-ndani-ya-moyo.html

No comments:

Post a Comment