Mwanaume hubadilika kwa mwanamke ambaye anamtaka na si kwa mwanamke mvumilivu. Ni jambo la kawaida kumuona mwanamke akivumilia mateso kutoka kwa mwanaume kwa miaka nenda miaka rudi, lakini wakiachana basi unakuta mwanaume anapata mwanamke mwingine na anabadilika mpaka unakuja kushangaa kama huyu huyu au mwingine?
Lakini wewe ambaye umeachwa unawaza kama alikua anakufanyia makusudi au la? Unajiona labda una mikosi au wewe ndiyo ulikua tatizo, hapana ishu haiku hivyo ishu nikuwa hukua fungu lako na ulikua unajilazimishia kwake. Najua unajijua, kama unajilazimishia unajijua, kama unaona hakuna kitu unachokifanya kikamfurahisha basi jua unajilazimishia.
Kama kila sikua anabadilisha wanawake na hajali kama umejua au la, kama kila siku ni kukupiga na ukiongea kidogo utasikia tuachane unajikuta unaomba msamaha kweli, kama kila siku wewe ni wa kulia kwenye mahusiano, kama hata siku moja haoni kitu kizuri unachomfanyia ni kukutukana na kukunyanyasa basi jua kua wewe ni wakulazimishia. Jua kwamba hata kama hataki kukuaacha lakini wewe si fungu lake.
Utavumilia na kweli ataendelea kubaki na wewe mpaka pale ambapo atakutana na mwanamke wa fungu lake huyu atampenda, hatampiga wala kumnyanyasa, hata akijamba utasikia umejamba vizuri atajichekesha kama fala na watu wataanza kusema kuwa kalishwa Limbwata. Lakini ukweli nikuwa wame ‘click’ na wanafuraha ndiyo maana makosa yake anayaona ya kawaida wakati wewe kunyenyekea kwako aliona kama matapishi.
Sasa Dada yangu uamuzi ni wako, uendelee kuvumilia mateso ukisubiri apate mtu wa fungu lake akuache au umuambie hapana inatosha na wewe utafute wa fungu lako. Labda nikupe moyo tu kuwa anaweza kukosa mtu wa fungu lake akaendelea kukunyanyasa wewe mpaka uzee. Ndiyo kuna watu wana miaka 20 kwenye ndoa bado wananiomba ushauri kua wananyanyaswa na kupigwa kila siku hawana furaha, nawewe vumilia utakua mmoja wao!
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/ukweli-mchungu-kama-mwanaume-si-wa.html
No comments:
Post a Comment