Sunday, March 22, 2020

SUALA LA USAWA KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE NI KITENDAWILI KISICHO NA MAANA

HILI SUALA LA USAWA SILIPENDAGI MIMI MAANA HALINA UPAKO WA MUNGU NDANI YAKE BADO LINAMAPUNGUFU KIBAO
TWAPIGANIA USAWA WA KIJINSIA "WA NINI"
Suala la kuwekeza katika kumfanya MWANAMKE apambane na kuwa na elimu yake, kazi yake, ajira yake, biashara zake na mkwanja wake, ni jema sana. Lakini ikiwa hatutawekeza kwa bidii katika kuwafanya WANAWAKE wawe watii na wanyeyekevu kwa WAUME zao(na kuthamini jinsia ya KIUME kwa ujumla) hapo tunakuwa tukiiteketeza jamii. Idadi ya WANAWAKE waliofanikiwa ambao hawaoni thamani ya kuishi na WANAUME inaongezeka kwa kasi ya ajabu. Lakini umekuwepo mtindo wa wengi wao kutaka kuzaa na kuendelea na maisha yao na u SINGLE (U MAMA wao). MWANAMKE alieamua kuwa SINGLE MAMA kwa makusudi huku akipuuza nafasi ya BABA maana yake ni kwamba kama anamtoto wa KIKE kutatengenezwa MWANAMKE mwingine "KIMEO". Kama ana mtoto wa KIUME maana yake kutatengenezwa MWANAUME "kimeo" asiejiamini na ambae hawezi kuja kumudu kuishi na MWANAMKE na kujenga familia. Siku hizi mabinti miaka yako ikishaanza kusoma 30+ ama kukaribia, na wakawa hawana uhakika wa "WAOAJI" haraka haraka wanapata mawazo ya "KISHETANI" kuzaa na kujidai KUWA wawe BUSY na maisha Acheni ujinga, mnajifanya muwe BUSY na maisha wakati TENDO la NDOA mnaendelea kulihitaji,(kama sio kufuga uasherati na kuhamasisha uzinzi ni nini hicho) na wengi wenu mnaishia kuiba WAUME za watu (kwa madai kuwa WAUME za watu sio wasumbufu) ilhali huko ni kuvuruga NDOA za wale waliopata fursa ya kuolewa Nyieeeeeee, ole wenu Tatizo sio WAOAJI tatizo ni WAOLEWAJI, maana kuna MWANAUME gani mjinga atajichomeka kuoa binti ambae ANASUMU za "USAWA wa kijinsia na UANAHARAKATI" ambazo ameanza kumezeshwa tangu FORM ONE mpaka chuo kikuu Utafiti nilioufanya nimebaini kwamba MWANAMKE yeyote awe ameolewa ama laa, ikiwa ana VINYEMELEA vya kutaka ama kujifanya mpigania "usawa wa kijinsia na haki za MWANAMKE" (wengi wao,) huwa ni WATATA sana(na huwa hawajijui kuwa mitazamo yao ni KERO kwa WANAUME) na wanaume "wanaojichomeka" kuwaoa cha moto huwa wanakiona. Ukumbuke hakuna MWANAUME(kwa asili) ambae yuko tayari ama anaeweza kuvumilia, kuishi na MWANAMKE anaetaka wawe sawa ama anaempandia kichwani. Mtanisamehe wanaharakati wa "usawa wa kijinsia", kwanza niko kinyume kabisa na suala la "usawa wa kijinsia", pili ninawakumbusha kwamba mnapofanya harakati zenu za kutafuta usawa muwe mnatathmini na athari za harakati zenu, maana naona Shetani anawatumia "vilivyo" kutuharibia mifumo ya familia na utu. Nimemaliza, na kama nimewaudhi nipelekeni dawati la jinsia kituo chochote cha polisi
Dr NAOMi


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/suala-la-usawa-kati-ya-mwanaume-na.html

No comments:

Post a Comment