Somo hili linaweza kukushangaza msomaji wangu, kutokana na ukweli kwamba ufanyaji mapenzi, hauwezi kuupangia muda, lakini katika hali ya kawaida ipo tofauti kubwa ya kufanya mapenzi, mchana, usiku, alfajiri na nyakati za joto na kelele nyingi za wapita njia.
Utofauti huu ndiyo unaweza kutofautisha hali ya kufurahia tendo kati ya mtu na mtu. Hakuna ubishi kwamba watu wanaofanya mapenzi nyakati za joto, hupoteza msisimko wa tendo si tu kwa sababu ya kuchoka haraka bali hata kwa kukinai harufu ya jasho liwatokalo mwilini.
Sababu hiyo na nyingine nyingi, zitokanazo na kutojua muda sahihi wa kufanya tendo la ndoa, zimewafanya wapenzi wengi kushindwa kuridhika au kupata raha stahili wakati wa kujamiiana na wapenzi wao, jambo ambalo linanipa sababu ya kufundisha muda sahihi wa kufanya mapenzi ni upi?
Kwa mujibu wa uchunguzi wangu, nilibaini kuwa muda muafaka wa wapenzi kufanya tendo la ndoa na kufurahia ni kati ya 9:30 na saa 4:30 usiku, Muda ambao zaidi ya wanawake 3,000 waliowahi kuhojiwa kwenye utafiti ulioripotiwa na mtandao mmoja hivi karibuni walikiri kuwa ufanyaji tendo la ndoa huwa na msisimko zaidi.
Hata hivyo, muda huo ulikubaliwa na wengi si tu kwa sababu una utulivu wa hali na mazingira, lakini pia ni wakati ambao hisia za mapenzi huamka kwa watu ambao pengine walikuwa na majukumu ya kazi mchana kutwa. Ukichunguza utabaini kuwa wanandoa wengi nyakati hizi huwa faragha na hata mafumanizi mengi hutokea kati ya saa 3 na saa 4 usiku.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/muda-sahihi-wa-kufanya-tendo-la-ndoa-ni.html
No comments:
Post a Comment