Sunday, March 1, 2020

Mapenzi bwana ni UCHIZI๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Image may contain: 1 person, standing and outdoor, text that says "Tu เค•ी เคœाเคจे pyar mera"
Yaani Mtu unamkamata Mwenza wako kakusaliti japo kwa kuhisi ama umeambiwa wala hujashuhudia kwa macho yako ETI UNAAMUA KUMUACHA kwa kujua kwamba AMEKUUMIZA.
Usivyo na FIKRA PEVU unaamua kuanza kusaka Mtu mwingine na unapokutana nae etiiii;
"HUYO NDIYE AMEKUJA KUTIBU JERAHA ZAKO" ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
kwa muda unajifanya kumuona yule wa Mwanzo ni SHETANI. Nani alikwambia MALAIKA WANAYAJUA MAPENZI?
Kumbe tumuite nani huyo ulompata kama sio UMEMPATA MALAIKA? Jilani yangu ngoja nikupashe HABARI tena kaa chini nipate kukuelezea vizuri, Bin adam yeyote ni Mkosefu ndiyo maana TU WADHAIFU kikubwa ambacho MUNGU alipenda kukiona kwetu ni UPENDO๐Ÿ’ž
Juu ya makosa hakuna ambaye hakuwahi kukosea bali tunajivika UTU ili kusameheana na kuinuana ki IMANI ili kukwepa yale ambayo tulikosea Mwanzo, Unapompa MWENZA WAKO NAFASI YA PILI unakuwa umemfundisha kwamba HAPASHWI KUKOSEA TENA na nikwambie kweli kabisa;
"KAMA ALIJUA KOSA LAKE HUYO NDIYE ATAKUWA MWAMINIFU"
Hata kama hatakuwa MKAMILIFU lakini tambuwa wazi AJUAYE MAKOSA YAKE HUYO ANALO PENDO JUU YAKO lakini pia tambuwa kwamba ANAKUHITAJI MAISHANI MWAKE hivyo ukimuacha huyo Kumbuka kwamba UNAKWENDA KUANZISHA UHUSIANO MPYA je ni kipi unajinasibu nacho kwamba UTAKUWA UMEMPATA MALAIKA? Maana Malaika hawana makosa ni wakamilifu ndo maana ni HAZINA YA MUNGU.
Najua kinachokutesa ni kwamba KWANINI AKUSALITI? Lakini tambuwa kwamba UNAWEZA KUJA KUTAMANI BORA USINGEMUACHA kwa sababu ni asilimia ndogo sana kutokutana na tatizo kama hilo bali kilicho cha THAMANI ni kujua UNAPENDWA Mengine unayaacha kwenye UBIN ADAM ๐Ÿ‘ซ
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria ๐Ÿ”จ


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/mapenzi-bwana-ni-uchizi.html

No comments:

Post a Comment