Sunday, March 1, 2020

Kisa cha Wana NDOA


Jane na John walikuwa wameoana miaka 5 iliyo pita bila kupata mtoto,lakin maisha yao bado yalikuwa ya furaha sana.
Siku moja wakiwa wamekaa sebulen ,mlango uligongwa na Jane aliinuka kwenda kufungua na kukutana na mrembo.
Jane: karibu Dada,nikusaidie nini?
Mgeni: naomba kuonana na John kama yupo,maana nimeona gari yake nje anayo itumia siku zote
Jane ( anashituka): umeijuaje kuwa ni gari anayo tembelea mume wangu? Kwan we nani?
Mara John anasogea na kukutana na mrembo,anapata mshituko mkubwa sana..
John: we Ashura umefuata nn hapa? Hebu twende nje tuongee
Jane: mume wangu nin knaendelea? Huyu ni nan?
John: mke wangu rud ndan tutaongea vizuri.. We Ashura nimesema twende nje
Ashura; John siwez kuendelea na huu uongo,bora iwe wazi. Dada Mimi ni mpenz wake John na hapa Nina mimba yake.
Jane: (anacheka kwa uchungu) ahaa kumbe,John huu ndo upendo ulio niahid? Nashukuru sana.
Wakat mkewe karud ndan,John huku anamkumbatia Ashura kwa furaha kuweza beba mimba kisha wanaongea meng na Ashura kuondoka....
John anapo rud ndan anakuta mke wake yupo kupakia vitu vyake tayar kwa kuondoka.
John: waenda wap mke wangu?
Jane: nimpishe mwanamke aliye kubebea mimba,siwez ishi na msalit ntapata kesi... Ulikuwa na sababu gan za kumpa mimba?
John: mke wangu tumekaa miaka mingi bila mtoto,nilitaman kuitwa baba.
Jane: kama kuitwa baba kutakamilisha furaha yako basi sawa Mimi sina neno.endelea na huyo mwanamke.. Lakin kumbuka tuliapa kupendana na kuvumiliana kwa kipind chote.lakin leo hii we umekuwa tofaut.maisha mema
BAADA ya MIEZI 6 kupita
John na Ashura walikuwa wameanza kuishi pamoja na alipata uchungu na kujifungua mtoto wa kiume.John alifurah sana kukuona mtoto wake...lakin daktar alikuja na kadi yenye vipimo vya DNA ikaonekana mtoto hakuwa wa John. Kwa maana hiyo Ashura alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine.
Yangu pale waliachana na maisha ya John yalibadilika na kuwa ya ovyo sana. Siku moja akiwa anatembea alimuona mke wake wa zaman Jane tena akiwa na mimba kubwa tu.
John: habar za siku nying Jane? Naona una mimba tayar hongera sana.
Jane: Asante,VIP mtoto na mkeo wanaendeleaje?
John : ( anasikitika): tuliachana,kumbe hakuwa mtoto wangu,nawe leo una mimba ,kumbe Mimi ndo sina uwezo kumpa mimba MWANAMKE
Jane: Mimi niligundua toka mwanzo maana hospitali niliambiwa sina shida ya kizazi.nilikaa kimya sikutaka kukuchanganya,niliendelea kukupenda tu ila ukaniona mi Fala
John: naomba turudiane tulee wote hiyo mimba na mtoto
"Baby nishanunua kila kitu,twende"
Ilisikika saut ya mwanaume akiwa na mafurushi na kumbusu Jane shavun huku akipapasa tumbo lake.
Jane: huyu ndo mume wangu na baba wa huyu mtoto tumbon. Mume wangu huyu ni John mume wangu wa zaman
Brown: habar bwana John? Nafurah kukuona...ngoja niwapishe kidogo muongee
Jane: kwa nn upishe? Sina cha kuongea na huyu mtu.salam imetosha,washa gar tuondoke
Funzo
Mtoto ni muhim ktk ndoa lakin upendo ndo muhim zaid. Wapo wenye watoto lakin hawana aman na furaha ktk ndoa zao
Mwanamke kutobeba mimba huenda we ndi tatizo,pima kwanza ndipo uongee. Na ukiona upo sawa yeye ana tatizo isiwe kigezo kumkandamiza.
Unapo msalit mkeo jua hata huyo hawala yako nae anakusaliti. Hivyo unapo lea au kutunza mimba ya mwanamke au mtoto usijihakikishie kuwa ni damu yako. Mama ndo anajua baba halali ni yupi.
Kumbuka kuna wakat mwanamke huona bora ampakazke mtu mimba ambae angalau anaweza toa matunzo kwa mama na mtoto.
Muheshimu mkeo
Karibu Mbeya

Image may contain: 1 person


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/kisa-cha-wana-ndoa.html

No comments:

Post a Comment