Bin adam tuna tabia tofauti iwe kwa maumbile ama hulka za ki malezi, Upendo mwingi hugeuka kuwa teso kwa yule anayejitoa MWILI, AKILI NA MOYO WAKE kwa ajili ya kumpenda mtu... Sisemi TUSIPENDANE laa hasha๐คฆ๐พ♂ ni tendo linaloashiria UBIN ADAM japo hata viumbe wengine wanapendana Kwani hujawahi kuwaona kumbikumbi๐ฆ? Wapo watu hutamka NAKUPENDA kama ishara ya pumbazo kwa mwenza wake, Mtu anaweza kulia ama kujiuguza ukadhani MPENZI SI HUYU SASA lakini ni mhunzi wa MAPENZI FAKE๐๐ฟ♂
Kikubwa alichonacho pengine aliishajua NYOTA YAKO inapandisha maisha yake, Wakati unakutana nae hata muonekano hakuwa nao ila leo kila mtu anapomtazama anam-admare ๐ swali je anakumbuka alikotoka? Wengi wenye tabia hizo hujihesabia haki kwani wamejawa ubinafsi, Mtu anapokufanya DARAJA la mafanikio yake kamwe hatajwi kwa upendo bali ni kwa masrahi yake, Watu hao kila ukitaka kumuacha TARAJIA KUONA PIPA LA MACHOZI๐ญ
Lakini ukimpa kisogo tu ANAKUNG'ONG'A๐คฃ mtu huyo ni hatari kwa maisha yako Kwani iko siku ambayo haina jina ATAKUMWAGA HUTAAMINI Kwani anaweza kukuvumilia kwa sababu malengo yake hayajatimia ngoja atimize malengo yake utaita Mama na alishatangulia mbele za haki๐
Machozi hayatoki moyoni, Kilio cha kwikwii na huzuni nyingi hazitoki moyoni, MOYO wa mtu ni ficho la kile anachokipanga sasa wewe endelea kumuonea huruma mwenzio kwa masrahi yake aje atusue akumwage๐ป ujutie kumvumilia wakati huo mwenzio atakuwa ANAIPEPERUSHA BENDERA๐ฉ ya penzi jipya na mtu ambaye hata hakumuombea kwa MUNGU kwa mafanikio aliyopata huku wewe ukiachwa UNAPAUKA TU๐ kataa kuwa DARAJA LA MAFANIKIO Ya Mtu laa kama unaamini safari yenu ni moja, Muda ni mali isiyooza ila inapitwa na wakati, Sasa wewe endelea kubembelezwa ukidhani unapendwa kumbe mwenzio anatembelea NYOTA YAKO ๐
#Elista_kasema_ila_Sio_she
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/je-uliwahi-kuishi-kwenye-mahusianondoa.html
No comments:
Post a Comment