Vita dhidi ya umasikini kwa kiwango cha kaya mpaka Taifa kwa jumla, nidhamu naipa namba moja kama ni sababu ya ukamilifu wa kuyafikia malengo. Ili mtu aweze kuwa na mafanikio lazima ajijengee tabia njema yenye misingi wa uaminifu, uwazi, busara, ukweli, hekima na heshima na mengineyo ya kumpendeza na wanajamii husika.
Hakuna mafanikio katika biashara, masomo au karama yoyote pasipo kuwa na tabia njema yenye kuruhusu ushirikiano na wengine. Maadili mema ya imani, kuthamini vyako, vya wengine na kuheshimu muda inaweza kuwa njia njema ya kuyaelekea mafanikio.
Mwanzilishi wa saikolojia ya kisasa bwana Sigmund Freud aliwahi kutamka katika hadhara huko Vienna kuwa “Kijana asiye na nidhamu ni kichaa”. Alitoa kauli hio baada ya kufanya tafiti chanzo cha vijana kutumia vilevi na kuishi maisha yasiyo na maadili. Aliibuka na majibu ya kwamba ukosefu wa nidhamu katika kazi, masomo, karama ambayo anayo mtu au akikosa kuitumikia katika misingi ya tabia njema basi hugeuka kuwa na madhara makubwa na mwisho kabisa mtu anaweza kuwa kichaa. Uvumbuzi huu aliukamilisha kwa kufatilia kwa ukaribu vijana waliojihusisha na matumizi ya “Cocaine” na ambao walikosa nidhamu mwisho wao ukawa kujikita katika matumizi mabaya ya vilevi.
Mwenye nidhamu ana nafasi kubwa ya kufanikiwa jambo lolote la maendeleo. Hekima ni jambo la msingi sana katika shughuli za uzalishaji mali, hakuna anayeweza kuzalisha mali bila kushirikiana na wengine. Ushirikiano unahitaji hekima zaidi, bila ya hekima misigano haitakwepeka na lengo la maendeleo halita kamilika.
Nidhamu ya muda inachachu kubwa sana katika njia za kuyafikia maendeleo, ukiacha kuheshimu muda ulionao sasa ama ukautumia vibaya basi kesho yako itaandaliwa na changamoto za leo. Hivyo ni vyema sana kujijengea tabia njema katika kufanya mipangilio ya mambo.
Nidhamu ya fedha na nidhamu ya uvumilivu, nimeviainisha kwa pamoja fedha na uvumilivu kwa kuwa vijana wengi katika swala la fedha hurukwa na akili na matokeo yake baada ya wao kuziendesha fedha basi fedha huwaendesha wao. Vita dhidi ya umasikini yatakiwa uvumilivu unatakiwa kwa hali ya juu, hakuna mtu popote ulimwenguni aliyefanikiwa kwa kukata tamaa vile vile hakuna mtu aliyefanikiwa kwa kuendeshwa na fedha.
Katika uwanja huu wa nidhamu ya fedha na uvumilivu nimtolee mfano kijana wa kimarekani mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni mwekezaji katika mtandao pia ni mmiliki wa mtandao wa kijamii “Facebook”. Mark Elliot Zuckerberg alitumia busara zaidi kwani alizaliwa katika familia tajiri na alijikita katika utafuta wa mali yake na si mali ya wazazi wake kama tunavyojilemaza waafrika.
Fedha za wazazi zinaharibu maisha ya vijana wengi ulimwenguni, wazazi wapatapo mafanikio basi mafanikio yale huwa ni sumu kwa familia kwani mali pasipo nidhamu huleta maafa kwa makuba hsa kwa vijana katika ya umri wa miaka 21 hadi 35.
Rejelea watoto wa wafalme Afrika, watoto wa matajiri na watoto wa masikini wanalioadhiliwa na maisha ya anasa. Ukosefu wa nidhamu kwa vijana huleta tama na starehe za zisizokubalika katika jamii. Mwisho wa kundi hili huwa ni mwisho mbaya kwani nidhamu inaposekana na usikivu hukosekana pia.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/hivi-unajua-kwamba-mwenye-nidhamu-ana.html
No comments:
Post a Comment