Saturday, May 2, 2020

WANAUME HATUAMINI KAMA KUNA URAFIKI WA MWANAMKE NA X WAKE, KAMA HUTAKI KUACHIKA KATA MAWASILIANO NAYE!

Simulizi nzuri Za Kiswahili Julkinen ryhmä | Facebook
Mume wako akigundua kuwa bado una mawasiliano na X wako, bila kujali ni mawasiliano ya namna gani, unampigia simu mnaongea, mnakutana na ni marafiki, kwanza hatakuamini hata kama hamna kinachoendelea. Pili atakuonya na kama hutasikia atakuacha, ndiyo atakuacha. Najua wewe mwanamke unaweza hata kumfumania na X wake ukamsamehe lakini mumeo hatasubiri hata akufumanie, akikuta meseji mnakumbushiana ujinga wenu wa zamani atakutimua.
Sasa dada yangu kabla hujaanza kusema kuwa nimarafiki tu, jiulize mara mbili je upo tayari kuharibu ndoa yako kwasababu ya “Rafiki tu” kibaya zaidi nikuwa huyo X wako siku akisikia umeachika hata kama ni kwasababu yake atakata mawasiliano. Ndiyo atakata mawasiliano kwakua sasa utakuwa huru, utaanza kuwa ‘mzigo’ wake hivyo hata kama hutataka lakini yeye atahisi kwamba utataka akuhudumie. Niukweli mchungu lakini ndiyo ukweli, acha mazoea na X wako!
Kama ameshakua X bila kujali sababu za kuachana kwenu hata kama mlijiambia kuwa mmeachana kwa wema ni X tu, atakuharibia ndoa yako. Ndiyo hata mimi nikigundua bado mnawasiliana halafu hakuna hata mtoto nitakuonya na usipo sikia uamuzi ni uleule. Hakuna namna nitakuacha, nikitu rahisi tu, huwezi kumchekea mtu ambaye ana ufunguo wa kitasa cha mlango wako. Kwamba eti useme ni rafiki tu hataiba uache hela zako hovyo hovyo, X wako alishakupata mara moja sitaki akupate tena.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/wanaume-hatuamini-kama-kuna-urafiki-wa.html

No comments:

Post a Comment