Tuesday, May 19, 2020

MWANAMKE LIJUE HILI LITAKUSAIDIA:


1.Mwanamke anapaswa kuwa na maisha yake na sio maisha ya kuiga. Wapo wanawake ambao hupenda kuiga kile kinachofanywa na wanawake wenzake na kudhani hivyo ndivyo anavyopaswa kuwa.
2.Mwanamke anapaswa kuwa mtiifu na mwenye heshima na pia mwenye busara.
Mwanamke hapaswi kuwa na kiburi na kutaka kuota mapembe ndani ya mahusiano. Heshima na utiifu haimaanishi kuwa tayari kunyanyaswa, hapana.
3. Mwanamke anapaswa kuwa na uwezo wa kujitegemea. Hapa utata idogo, wapo wale wanaoamini kuwa mwanamke anapaswa kutegemea kila kitu toka kwa mwenza wake.
(Wanaume hawapendi Mwanamke golikiba)
4.Mwanamke lazima awe anajiamini.
Naam, hapa haimaanishi kuwa anatakiwa kuwa kiburi na mbishi, hapana. Isipokuwa mwanamke anapaswa aonyeshe kujiamini kwa kile anacosema na anachotenda.
5. Mwanamke anapaswa kuwa na mvuto.
Hapa haimaanishi kuwa mrembo saaaana, hapana. Ina maana kuwa mwanamke anapaswa kuwa nadhifu kila wakati ili kumfanya mwanaume apende kuwa nawe na avutiwe kuwa nawe wakati wote.
6.Mwanamke anapaswa kuwa Mcha Mungu.
Wanaume wanamin kuwa mke akijiweka karibu na Mungu ni ngumu kuingia ktk Mambo mabaya.
7.Wanaume wanapenda mwanamke atakaye wapenda watu wa nyumban mwake. Mwanamke mwenye upendo na ndg wa mme (wazazi) huyo ndiye mwanamme hupenda.
Sifa hizi akiwa nazo mwanamke, basi atambue fika kuwa Mwanaume atavutiwa nawe na uhusiano wenu unaweza kudumu na kudumu na kudumu zaidi.
Kujiunga na group letu la semina za ndoa na Familia WhatsApp Link hii.👇
https://chat.whatsapp.com/BAghEHWmUxP8AvcefqRfGN


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/mwanamke-lijue-hili-litakusaidia.html

No comments:

Post a Comment