Wednesday, May 27, 2020

WANAWAKE WENGI SIKU HIZIMNAKWAMA HAPA

Wanawake wengi mno mnakwama hapa👉kiauhalisia hakuna mkamilifu hapa chini ya jua kila mmoja ako na mapungufu yake na hadi imefika mahali umeolewa na huyo mwanaume kama kweli ulielewa Nshetani hukufata harusi basi uliyaridhia madhaifu yake na yeye akayaridhia yakwako.,
Hatuolewi na kakazetu Bali watoto Wa wanawake wenzetu ambao kila mmoja kalelewa kivyake hivyo madhafu yetu hayafanani ,na unapoingia ktk hili agano jiandae kisaikokojia kwamba katika hiyo Ndoa kutakua na vipindi vitatu tofauti ambavyo kila mmoja kati yenu ajiandae kuvipitia hivi ata kiongozi wako Wa dini amevipitia au anavipiti,DHIKI ,MAUMIVU NA CHUKI ,kuna wakati mmoja katiyenu ataibua kisirani kisichoeleweka au kavurugu flani hali itakayo mpelekea kutamani kuwa nnje ya wewe kwa muda .
Hali hii haimaanishi hakupendi ila tuu hutokea automatic sasa itategemea utaihendo vipi kama utaona kuelezea ndugu ndio suluhu au marafiki utaharibu zaidi wakati huu ndio wanaume wengi huamua kuenda na mpango Wa kando coz upande wetu sisi wanawake huwa tunakua mbogo kelele kama tumemeza radio ,mana akianza kuchelewa kurudi tayari ngumu kuvumilia kwa wanawake wengi,niseme hivi kama huna uwezo Wa kumuacha mwanaume usitangaze mabaya yake tumia muda huo kuwa bz na mambo mengne upepo upite huku ukiomba .
Imetokea umemfumania mumeo unapiga ukungu kuwajulisha wengne kwamba mumeo ni Malaya wakati unajua fika kwamba huna jeuri ya kutoka hapo ,tumia hekima kulimaliza wanaume wengi wanafanya matukio kwenye fumanizi na kujiua au kuua coz wao hawawezi kutangaza kwa jamiii ,..
Kakazangu atakama unaona shetani anakupitiaga kwa mpango Wa kando usimuonyeshe mwenzio ni dharau kubwa mno wengne huleta uasherati huu hadi kwa nyumba mnazoishi na wake zenu huo ni udhaifu mkubwa mno na ukatili Wa hali ya juu ,kama unamwamini Mungu unadini unajua zinaa ni dhambi jitahidi kumshinda shetani huko nnje hakufai makahaba wamekua washirikina ukiingia kwake unasahau mke na watoto ,hii kwa wanawake pia usitoke nnje ya mwenzio wala usishindane na mwanaume coz tangu zama za kale hakuitwa Malaya ila mwanamke mnazini wote mawe unapigwa mwanamke,usishindane na mwanaume kwa usalama Wa Ndoa yako.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/wanawake-wengi-siku-hizimnakwama-hapa.html

No comments:

Post a Comment