Thursday, May 28, 2020

WANAWAKE JUENI TOFAUTI KATI YA 'NATAKA NIKUOE' NA 'NATAKA UNIZALIE' NAONA MNACHANGANYA SANA!

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Kuna tofauti kati ya ‘Nataka Nikuoe’ na ‘Nataka Unizalie’ wadada mnaonekana kuchanganya sana haya mambo mtu kakuambia ‘Nataka Unizalie’ ukishabeba mimba unaanza kuuliza ‘Unakuja lini kujitambulisha’ kwani bila kuja kwenu mtoto hapumui?
Kuna wanawake wengi ni ma single mother hii leo kwakua wameshindwa kuelewa kuwa Mwanaume anapoesema “Nataka Unizalie” hamaanishi kuwa anataka kukuoa, wala haimaanishi kuwa anataka uwe mpenzi wake, wala haimaanishi kuwa anakupenda. Yeye anachotaka ni mtoto tu, yaani mwanaume wa namna hiyo hana mpango na wewe kungekua na uwezekano abebe mimba yake angeibeba mwenyewe. Mwanaume anayetaka kukuoa anakuambia anataka kuja kwenu, unampeleka, anatoa mahari anakuoa. Anayetaka mtoto hahitaji hata kukujua jina la kweli achilia mbali kuwajua wazazi wako!
Najua inauma lakini ndiyo ukweli, sisemi hatakuoa lakini hakukudanganya, alikuambia anataka mtoto ushampa kaa utulie akikutaka na wewe atakuambia. Hapa najua sauti inatosha ila mnauchuna tu kama vile hamsikii.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/wanawake-jueni-tofauti-kati-ya-nataka.html

No comments:

Post a Comment