Thursday, May 21, 2020

EO TUNAWAOMBEA WANAUME


Hatuwaombei kwa sababu sisi ni watakatifu kuliko wao au sisi hatuna dhambi au madhaifu yetu
Lakini tunawaombea kwa sababu ni baba zetu, ni kaka zetu, ni waume zetu, ni watoto wetu na iwe tunataka au hatutaki hatuwezi kuwaondoa kwenye maisha yetu
Tunawaombea toba na rehema
Wasamehe, wahurumie
Samehe uovu wao
Samehe ujeuri wao
Samehe ubabe wao
Samehe usaliti wao
Samehe dharau zao
Samehe uongo wao
Samehe manyanyaso yao
Samehe walipokua wazembe na hawakutunza familia kama inavyopasa maana neno lako linasema asiyetunza wa kwao ni mbaya kuliko asiyeamini.
Samehe Yesu, samehe
Inawezekana uchumi wa familia nyingi unapigwa kwa sababu yao
Inawezekana magonjwa ya zinaa yameingia kwenye familia nyingi kwa sababu yao
Inawezekana umasikini na madeni vimeingia kwenye familia nyingi kwa sababu yao
Inawezekana magonjwa ya presha, stress, kansa yameingia kwa wake zao na mama zao sababu ya uchungu na maumivu waliyowasababishia.
Inawezekana wanaomba na maombi yao hayajibiwi kwa sababu kuna wanawake wanalia kwa ajili yao
Inawezekana ardhi yao yenye rutuba imegeuka udongo wa chumvi usiozaa na mbingu juu yao imegeuka shaba sadaka na maombi yao havipenyi kwa sababu ya maumivu waliyosababishia watu.
Samehe Yesu.
Ona rehema Bwana
Usiangalie machozi ya wanawake yaliyojaa kwenye madhabahu yako.
Wakipigwa wao familia zinaumia pia.
Rehemu wanaume wa Tanzania, wasamehe, wape mwanzo mpya
Neno lako katika Malaki 2:13‭-‬16 linasema
Zaidi ya hayo yote, mnaifunika madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kwa machozi yenu, mkilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena sadaka mnazomtolea. Mnauliza, “Mbona sasa hazikubali?” Mwenyezi-Mungu hazikubali kwa sababu anajua wazi kuwa umeivunja ahadi yako kwa mke wa ujana wako. Umekosa uaminifu kwake ingawa uliahidi mbele ya Mungu kwamba ungekuwa mwaminifu kwake. Je, Mungu hakuwafanya nyote wawili muwe mwili mmoja na roho moja? Je, alikusudia nini alipofanya hayo? Yamkini alikusudia tuzae watoto ambao watamcha yeye. Kwa hiyo, hakikisheni kuwa hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe. Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema: “Ninachukia talaka. Ninachukia mmoja wenu anapomtendea mkewe ukatili huo. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.”
SAMEHE YESU
ONA REHEMA
NA SISI TUSAIDIE KUWASAMEHE
NA WAO WAPE KUTUSAMEHE
REJESHA WANAUME WA TAIFA HILI KATIKA MSTARI
KOKOTE SHETANI ALIKOWAVUTA YESU WACHOMOE WARUDISHE KATIKA JINA LA YESU, AMEN.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/eo-tunawaombea-wanaume.html

No comments:

Post a Comment