Monday, May 25, 2020

EWE MWANAMKE MTUMIE UJUMBE HUU MUMEO ALIYE KAZINI.

utamuzaidiapp
πŸ’žπŸ’ž
*DARASA LA MAHUSIANO*
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi
πŸ’žπŸ’ž
Salamu yako ni nusu ya uhai wangu, kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi yangu, kuipata nisawa na ua ridi machoni mwangu, nakila ninapoipata huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana Muhibu wangu.
πŸ’žπŸ’ž
Mchana wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. MCHANA MWEMA.
πŸ’žπŸ’ž
Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia, fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu, fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo kwa kukutumia sms mpenzi wangu, Nakutakia usiku mwema.
πŸ’žπŸ’ž
Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo kama ukiwa mbali "NIACHE NIKUPENDE SWEET"
πŸ’žπŸ’ž
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! "NAKUPENDA MALAIKA WANGU"
πŸ’žπŸ’ž
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu "SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO"
πŸ’žπŸ’ž
Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI
πŸ’žπŸ’ž
Mpenzi kila tunapokuwa chumbani huwa napenda kuwa mbunifu, huwa najitahidi kuepuka udhaifu, ili mapenzi yangu yasikukifu, ENDELEA KUFURAHIA MAPENZI YANGU. Mchana mwema.
πŸ’žπŸ’ž
Wewe ni wapekee ninaekupenda, sifikirii kukusaliti na wala sina wazo la kukutenda, nakuomba tuendelee kupendana siku zote habbity wangu.
πŸ’žπŸ’ž
Mapenzi ni matamu napia yana raha, wewe hauni ishi hamu, siku zote wanipa raha, wewe kwangu ni mtu muhimu, unaeng'aa moyoni mwangu kama nyota ya jaha. "NAKUOMBA USINIACHE MPENZI WANGU"
πŸ’žπŸ’ž
Dhamira kuu ya Moyo wangu ni Mapenzi, kukupenda kwa dhati bila kipingamizi, kuishi nawewe kihalali kwa kudra za wazazi, Nipende nikupende Tudumishe Mapenzi. "NAKUTAKIA MCHANA MWEMA MPENZI WANGU"
πŸ’žπŸ’ž
Yapate haya yote kwa kujiunga na group letu la facebook la UISLAMU CHAGUO LANGU na pia LIKE page yetu ya Habari za Kiislamu na Kutembelea account yetu ya Furaha ya Ndoa mara kwa mara inshaallaah.
Kazi kwako mwanamke....


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/ewe-mwanamke-mtumie-ujumbe-huu-mumeo.html

No comments:

Post a Comment