Wednesday, May 27, 2020

USIWE MTUMWA WA PENZI LA MTU ASIYEJALI KUJITOA KWAKO KWA KIWANGO UNACHOMPATIA.


Mtu anavyokufanya ujione kama HAKUHITAJI basi usiondoke kwake ili ajihisi hatia au asikitike maana hilo haliwezi kutokea.
.
Ondoka katika maisha yake kwa sababu kubwa moja tu, kwamba hujaona sababu yoyote yakuendelea kuwa na yeye au inayokufanya upiganie mahusiano hayo.
.
Inafika kipindi mtu lazima uwe na ujasiri dhidi ya hatima ya maisha yako kwa sababu jambo ambalo umeandikiwa kuwa nalo litakuwepo na kama hukuandikiwa haliwezi kudumu.
.
Ndio, Mahusiano yanafaa kupiganiwa lakini sio wewe peke yako unaetakiwa kupigania. Muda mwingine mtu unayempigania na yeye lazima azione jitihada zako na kuzithamini walau hata kidogo.
.
Kama hana muda huo, itoshe kutambua kwamba unachompa ni zaidi ya anachostahili.
.
Kuwa sehemu ambayo moyo wako unahisi unathamimiwa, jitihada zako zinaenziwa na mchango wako unatambulika. Sio sehemu ambapo unavumilia.
“Don’t try to force anything. Let life be a deep let-go. God opens millions of flowers every day without forcing their buds.”


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/usiwe-mtumwa-wa-penzi-la-mtu-asiyejali.html

No comments:

Post a Comment