Friday, May 29, 2020

MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI. BY DK.HABELNOAH


1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na
kikohozi.
2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri
yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio
(allergy).
3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa
kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi
mwilini.
4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango
cha tatizo la sukari mwilini.
5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye
matatizo ya nguvu za kiume.
6. Pia inatumika kama scrub ya uso.
Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi
na inasaidia kuondoa uchafu usoni.
7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa
ya kuponyesha tumbo la kuhara.
8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumia
majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri
kwa kupunguza maumivu na kukulinda na
maambukizi ya bakteria.
9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri
yanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa na
mdudu na kupunguza maumivu.
10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina
uwezo wa kutibu tezi dume.
11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi
majani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibu
chunusi.
12. Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguza
uzito mwilini na kuzuia uharibifu sukari ndani ya
mwilini.
13. Majani ya mpera yanajaza nywele na
kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la
kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha
kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka
chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya
nywele zako.
14. Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi,
maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mpera
na utaona maajabu ya majani haya.
15. Chukua majani ya mpera saga vizuri mpaka
yawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kisha
tumia kupaka usoni kama scrub inatibu ngozi
inayoanza kuzeeka mapema.
16. Chai ya mpera inasaidia kwa kutibu
mvurugiko wa tumbo.
Pamoja na majani hayo kuwa msaada wa kutibu
maradhi mbalimbali , halikadhalika juisi ya
mapera nayo husaidia sana kutibu mgolo au
bawasiri, figo na hata kuondoa mafuta katika
moyo.
Kimsingi mti wa mpera karibu kila sehemu yake
ni tiba kwani hata mizizi yake inapochemshwa na
kutumia kwa kunywa huenda kuwasaidia
wanawake wenye matatizo ya hedhi au wenye
matatizo ya kutokwa na maji yenye harufu
mbaya sehemu zao za siri.
AHSANTENI SANA……………
Usiache ku-SHARE na wengine wapate elimu hii.
Imeandikwa na DK.HABELNOAH


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/majani-ya-mpera-na-faida-zake-mwilini.html

No comments:

Post a Comment