Mtu anapokua mpenzi wako haimaanishi kwamba unammiliki? Mnapooana na mtu haimaanishi kwamba unammiliki! Haimaanishi kwamba hawezi kukuchoka! Haimaanishi kwamba ni lazima kuwa na wewe mpaka mmoja wenu atakapokufa! Haimaanishi kwamba hamtakiwi kuachana! Kuna kipindi mtachokana tena bila sababu, kuna kuachana na nikawaida.
Lakini tofauti ya ndoa na kuishi pamoja au mahusiano ya kawaida nikuwa, unapomchoka mtu kwenye ndoa si maamuzi yako peke yako tu kuachana. Kunakua na ndugu, kunakua na viongozi wa dini na jamii nzima kwa ujumla. Kwamba huwezi kuamka asubuhi tu na kusema leo namuacha mke wangu au mume wangu na watu wakakuchekea.
Hata kama tayari ushafanya maamuzi yako basi kuna watu watajaribu kuingilia kati, mnaweza kusuluhishwa na pengine kama ni makosa kila mtu akatambua yakwake akajirekebisha. Lakini katika mahusiano hilo ni jabo la watu wawili, ukimchoka mtu hata kama mmezaa naye unamuambia kwa heri.
Hata kama mlishaishi miaka kumi pamoja, kwakua hakuna kitu cha kiimani au kisheria kinachowaunganisha basi nirahisi kumuacha hivyo hivyo kwake nirahisi kukuacha na ni nadara sana watu kukaa vikao eti kujadili kuwa flani kamuacha mpenzi wake. Tena wakati mwingine hata hupewi taarifa kuwa umeachwa bali unashangaa kaoa au kuolewa na mtu
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/mtu-anapokuwa-mpenzi-wako-haimaanishi.html
No comments:
Post a Comment