Saturday, May 16, 2020

πŸ’œπŸ’œπŸ’œ*** HEKIMA HUJENGA NDOA YENYE FURAHA,

Mwanadada: DR LOVE
Kila mwanamke aliye mwema na hekima hujenga nyumba yake; Bali asiye na hekima hubomoa kwa mikono yake mwenyewe.kuna msemo usemao; majuto mjukuu"Nikawaida kwa wanandoa kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo,Matatizo mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata muongozo wa Allaah (sw) ,
1:πŸ’œπŸ’œπŸ’œ** sifa ya kwanza.hufumbua kinywa chake kwa hekima.na sheria ya wema katika ulimi wake.Wanawake wengi huwajui kuutumia ulimi vizuri !! Ukali maneno ya mikato,Matusi, Ukaidi n.k kwao ni mambo ya kawaida .Wengi wanatawaliwa na hasira na wivu ,akiona mwanamme kaongea na mwanamke asiyemjua ni kosa la jinai huenda ni mfanyakazi mwenzake hata hatumii busara kutakakuelewa matokeo yake mwanamke hufura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika kila mtu nyumbani wanatambua kuwa hali ni mbaya,
2; πŸ’œπŸ’œπŸ’œ*** Hufanya kazi kwa moyo na huamka alfajiri na mapema,Kuna wanawake ambao ni wavivu kupindukia.inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl , wanaume ni rahisi sana kuvutwa na anayemuhudumia kwa ukaribu.,House Girl akiandaa chakula,mata kitanda,mara maji ya kuoga,mara apige deki chumbani n.kHachelewi mwanaume kulipa fadhila kwa wema anaotendewa,
3:πŸ’œπŸ’œπŸ’œ** Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa famila yake,kuna wanawake ni wachafu-- Usishangae kukuta sufuria kwenye makochi,chumba cha kulala ni stoo ya nepi za mikojo na nguo chafu,wengi kuoga ni anasa.Mwanamke ni maji,sharti mwanamke awe msafi muda woteWanaume wote wanapenda usafi, marashi hata ya mchina yasikose, Mwanamke hakikisja ""reception "" inakuwa safi na kuwa katika hali ya kumfanya mume ajisikie kujipumzisha kwa Raha msyarehe.
4:πŸ’œπŸ’œπŸ’œ** Jali na timiza mahitaji ya (NDOA) Kwa mume wako,upo msemo umaosema Mwanamke mwema " Taa yake haizimiki usiku" ,Kuna wanawake wavivu kwa swala hili.pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma Utakuta wiki nzima mama apanda kitandani huku amevaa " KOMBATI: Utafikiri ni askari anaenda vitani.Wanaume ni sawa nambuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa, Fanya makosa yote. Lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya ndoa,hilo ni kosa la jinai,Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa,nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Allaah
5;πŸ’œπŸ’œπŸ’œ*** Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu,ambacho familia itafurahia.Wanawake wengi hasa wa zama hizi hawajui kupika,ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula Hotelini au kwa mama ntilie,tusione aibu kujifunza kwa watu namna ya kukangariza,Akina mama ni wajibu wetu kujifunza mapishi kuilelea ndoa.mchicha peke yake waweza kuwa na mapishi zaidi ya 10 Wanaume wanapenda chakula chenye ladha mfanye mume akumbuke chakula cha HOME,
6:πŸ’œπŸ’œ*** Mwamini mume wako,wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako.Usitoe siri za ndoa yenu kwa masjoga au ndugu zako.,muda wote muombe Allaah akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea Muombee mume wako ili Allaah amsaidie pia awe na hekima ya kutunzs ndoa kwa uadilifu na upendo


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/hekima-hujenga-ndoa-yenye-furaha.html

No comments:

Post a Comment