Friday, May 1, 2020

UREMBO/UTANASHATI WA MTU SIO KILA KITU KATIKA MAHUSANO.


Katika Ulimwengu Tulionao Kwa Sasa Wanaume Wengi Huangalia Urembo Wa mwanamke, Umbo Lake Na Ukubwa Wa Makali Wanapochagua Wanawake Wa kuanza Nao Maisha. Wengine Utawasikia Wakisema Ubora Wa Nyumba Ni Chuo Na Uzuri Wa Mwanamke Ni Kuwa na Makalio Makubwa.
Wanawake Nao Hupendelea Wanaume Watanashati Wanakwambia Hatutaki Mwanaume Mwenye Sura Kama Tafadhali Nipigie. Zaidi Sana Wanaangalia Mfukoni Mwa Mwanaume Ana Nini??
Mwonekano Wa Nje Na Uwezo Wa Kifedha Umekua Kipaumbele Kikubwa Baina Ya Vijana Wengi Ambao Wanaanzisha Maisha Katika Ulimwengu Wa Sasa au Wanao amua Kuoana.
Ila Ningependa Kukuambia Kaka Yangu, Unapochagua Mwanamke Tambua Kwamba Unachagua Mwanamke Ambaye Atakuwa Mama Wa Watoto Wako, Atakuwa Mwalimu Wa Watoto Wako Na Atakuwa Mfano Au kioo Watoto Wako watakitazama Pindi Wanapohitaji Kujifunza Au Kuchukua Mfano Wa Kuigwa.
Kwako dada Yangu Pesa Au Utanashati Wa mwanaume Haukuhakikishii Furaha Na Amani Katika Maisha Yako Ya Ndoa. Bali Upendo Na Kukujali Kwake Mwanaume wako Ndio Chimbuko La Furaha Moyoni Mwako. Kuwa na Mtu Atakaye Kuwa tayari Kukujali Wewe Na Watoto wako na kuwapa Muda wake.
UNAPO CHAGUA MWENZA WA MAISHA CHAGUA VYEMA MAANA UREMBO NA UTANASHATI SIO KILA KITU.
.
Image may contain: 1 person, outdoor


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/uremboutanashati-wa-mtu-sio-kila-kitu.html

No comments:

Post a Comment